RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge July 2024

Filed in Uncategorized, Ajira by on 20/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge July 2024

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge July 2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge 20-07-2024, Ajira Mpya Tume ya Utumishi wa Bunge July 20-2024, parliament of tanzania jobs,The National Assembly of Tanzania and the President of the United Republic make up the Parliament of Tanzania.

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge July 2024

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge July 2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge 20-07-2024, Ajira Mpya Tume ya Utumishi wa Bunge July 20-2024, parliament of tanzania jobs,The National Assembly of Tanzania and the President of the United Republic make up the Parliament of Tanzania.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeundwa kwa mujibu wa Ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Aidha, Ibara ya 88 ya Katiba inaunda Sekretarieti ya Bunge yenye jukumu la kuliwezesha Bunge kutekeleza majukumu yake. Kwa msingi huo, Sekretarieti ya Bunge, inatangaza nafasi za kazi za Kada mbalimbali ili kuimarisha utendaji wake.

Watanzania wote wenye sifa na uwezo
wanaalikwa kutuma maombi yao ili kujaza nafasi za kazi kama zilivyoainishwa hapa chini:-

Nafasi za kazi Tume ya Utumishi Wa Bunge Tanzania

✅AFISA TAWALA DARAJA LA II – NAFASI 1

KAZI NA MAJUKUMU YA AFISA TAWALA DARAJA LA II

  • Kusimamia kazi za Utawala na Uendeshaji katika Taasisi;
  • Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu mbali mbali za Taasisi;
  • Kuainisha, kuchambua na kushauri kuhusu mahitaji ya vitendea kazi
    kwa watumishi;
  • Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu ya Taasisi;
  • Kusimamia/kuratibu utoaji wa vitambulisho kwa watumishi; na
  • Kazi zingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Shahada kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na
Serikali katika fani ya Utawala, Menejimenti ya Umma na awe na Ujuzi wa kutumia Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni PSS D

✅FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UMEME) – NAFASI 1

KAZI NA MAJUKUMU YA FUNDI SANIFU UMEME DARAJA LA II

  • Kukagua na kuripoti kasoro za kiufundi za mifumo ya umeme (Electrical Faults);
  • Kushughulikia kasoro ndogo ndogo za kiufundi za mifumo ya umeme;
  • Kufanya usanifu na kupendekeza miradi midogo midogo ya umeme;
  • Kufuatilia na kuhakiki ankara za umeme; na
  • Kazi zingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Stashahada (Diploma) katika fani ya Fundi Umeme
kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni PSS C

✅FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UFUNDI) – NAFASI 1

KAZI NA MAJUKUMU YA FUNDI SANIFU MITAMBO (MECHANICAL TECHNICIAN)
DARAJA LA II

  • Kufanya ukaguzi wa ubora wa magari, mashine na mitambo na
    kushauri ipasavyo;
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya magari, mashine na mitambo;
  • Kuandaa taarifa za kiufundi za magari, mashine na mitambo na kuziwasilisha kwa msimamizi wake wa kazi;
  • Kuandaa Mpango wa Matengenezo Kinga ya magari, mashine na mitambo; na
  • Kazi zingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Stashahada (Diploma) katika fani ya ufundi mitambo
kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni PSS C

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge July 2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge 20-07-2024, Ajira Mpya Tume ya Utumishi wa Bunge July 20-2024, parliament of tanzania jobs,The National Assembly of Tanzania and the President of the United Republic make up the Parliament of Tanzania.

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Bunge July 2024

✅MTEKNOLOJIA DAWA DARAJA LA II – NAFASI 1

KAZI NA MAJUKUMU YA MTEKNOLOJIA DAWA DARAJA LA II

  • Kuainisha, kuandaa na kuagiza mahitaji ya dawa na vifaa tiba katika eneo lake la kazi;
  • Kugawa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa kulingana na maelekezo ya Daktari;
  • Kuchanganya na kutayarisha dawa;
  • Kuhifadhi dawa na vifaa tiba;
  • Kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa;
  • Kukagua dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika eneo lake la kazi;
  • Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa;
  • Kuandaa taarifa ya matumizi ya dawa na vifaa tiba;
  • Kufanya uchunguzi wa ubora wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi;
  • Kufanya kaguzi mbalimbali katika sehemu zinazohifadhi dawa;
  • Kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba; na
  • Kazi zingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Stashahada (Diploma) ya Uteknolojia ya muda wa miaka
mitatu (3) katika fani ya dawa kutoka Chuo cha Afya kinachotambuliwa na
Serikali, awe amesajiliwa na Baraza la Famasi pia awe na Leseni hai ya
kazi.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGHS B

✅TABIBU WA KINYWA NA MENO DARAJA LA II (DENTAL THERAPIST) –
NAFASI 1

KAZI NA MAJUKUMU YA TABIBU MENO DARAJA LA II

  • Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida ya kinywa na meno;
  • Kuziba na kung’oa meno;
    iii) Kushiriki katika kupanga na kutekeleza Huduma za Afya Msingi;
  • Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma;
  • Kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji; na
  • Kazi zingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe mwenye Stashahada (Diploma) ya Tabibu wa Meno kutoka
Chuo kinachotambuliwa na Serikali, pia awe amesajiliwa na Baraza la
Madaktari na awe na Leseni hai ya kazi.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGHS B

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu waliopo kazini serikalini.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika Kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na.CAC.45/257/01/D/140 wa Tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika na picha (passport size) ya hivi karibuni.
  • Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa
    wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi zinazohusika kama vile: –
     Shahada (Degree), Stashahada ya Juu (Advanced Diploma), Stashahada (Ordinary Diploma) na Astashahada (Basic Certificates);
     Cheti cha Mafunzo ya Kompyuta (Computer Certificate); na
     Vyeti vya Kitaaluma vinavyotolewa na Bodi/Taasisi zinazosimamia taaluma
    (Professional certificates from respective boards).
  • Hati za Matokeo za Kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI Result Slips) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji wawe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho hicho.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
    vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka zinazohusika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji wawe hawajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai.
  • Waombaji waliostaafishwa au kuacha kazi katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba, isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi watakaowasilisha taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 02 Agosti, 2024.

MUHIMU
Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Barua hiyo ielekezwe kwa: –
KATIBU WA BUNGE
OFISI YA BUNGE
10 BARABARA YA MOROGORO
S.L.P. 941
40490 TAMBUKARELI
DODOMA.

Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: – http://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Kwa msaada na ufafanuzi piga namba; +255738685177. Simu zipigwe muda wa
kazi kuanzia Saa 2:00 Asubuhi – 11:00 Jioni.

KUTUMA MAOMBI CHAGUA KADA YAKO HAPA CHINI!

  1. NAFASI za Mteknolojia Dawa Bungeni July 2024
  2. NAFASI za Afisa Tawala Bungeni July 2024
  3. NAFASI za Fundi Sanifu Umeme Bungeni July 2024
  4. NAFASI za Fundi Sanifu Mitambo Bungeni July 2024
  5. NAFASI za Tabibu wa Kinywa na Meno Bungeni July 2024

DONWLOAD PDF DOCUMENT

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , , ,

Comments are closed.