RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama July 06-2024

Filed in Ajira by on 06/07/2024

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama July 06-2024

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama July 06-2024

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama July 06-2024

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama July 06-2024, Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Aidha, Ibara ya 113 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Sura 237 vinaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama majukumu mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuajiri watumishi wa Mahakama ya Tanzania wa kada mbalimbali.

Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa
zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi Mahakama ya Tanzania katika Mikoa na Wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi:

HAKIMU MKAZI II – TJS II

SIFA ZA KUINGILIA:-
Waombaji wawe na Cheti cha kuhitimu kidato cha Nne/Sita, Shahada ya Sheria
“Bachelor of Laws” (L.L.B) kutoka Vyuo Vikuu au Taasisi za Elimu ya Juu
zinazotambuliwa na Serikali pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Mafuzo ya
Sheria kwa Vitendo Kutoka Shule ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (The Law school of Tanzania). Wenye cheti cha kuhitimu mafunzo ya kompyuta
watapewa kipaumbele.

KAZI ZA KUFANYA:-

  1. Kuandaa mpango wa kusikiliza mashauri ya awali ya mashauri ya
    Jinai na Madai;
  2. Kusikiliza mashauri ya awali ya Jinai na Madai;
  3. Kusikiliza mashauri ya awali ya ndoa na mirathi;
  4. Kuandaa na kutoa hukumu kuhusu mashauri yote aliyosikiliza;
  5. Kutoa amri mbalimbali za kimahakama anazoruhusiwa kisheria;Kusuluhisha mashauri;
  6. Kusikiliza rufani kutoka Mabaraza ya Kata;
  7. Kufanya utafiti wa kisheria na kutoa ushauri; na
  8. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na msimamizi wake

✅AFISA HESABU II – TGS. D

SIFA ZA KUINGILIA:-
Waombaji wawe na mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini;-

  • Wenye “Intermediate Certificate” (Module D) inayotolewa na
    NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na
    NBAA, au
  • Shahada ya Biashara/Sanaa aliyejiimarisha kwenye fani ya
    Uhasibu, au
  • Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Taasisi yoyote
    inayotambulika na Serikali.

KAZI ZA KUFANYA:-

  • Kushiriki kuandika taarifa ya mapato na matumizi
  • Kushirikiana na Mhasibu kuandaa taarifa za maduhuli
  • Kushiriki kufanya usuluhisho wa hesabu za benki na nyingine
    zinazohusiana na masuala ya fedha.
  • Kuandaa taarifa mbalimbali za mishahara
  • Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi
  • Kutunza daftari la amana
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake
    wa kazi.

✅MSAIDIZI WA HESABU I – TGS. C

SIFA ZA KUINGILIA:-
Waombaji wawe na mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini;-

  • Wenye Stashahada ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambulika na
    Serikali. Au
  • Wenye Cheti cha ATEC II inayotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.

KAZI ZA KUFANYA:-

  • Kutunza daftari la fedha la matumizi ya kawaida na maendeleo.
  • Kutunza nyaraka za hati za malipo.
  • Kuingiza mapato na matumizi kwenye vitabu vya fedha.
  • Kuandika taarifa mbalimbali za fedha zilizopokelewa.
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake
    wa kazi.

✅AFISA UTAWALA II – TGS D

SIFA ZA KUINGILIA:-
Waombaji wawe na Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:- Utawala, Elimu ya Jamii,
Sheria (Baada ya internship), Menejiment ya Umma, Uchumi na wenye na ujuzi wa kutumia kompyuta.

KAZI ZA KUFANYA:-

  • Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu.
  • Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu
    mbalimbali.
  • Kusimamia kazi za utawala na uendeshaji katika Ofisi za Serikali.
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake atakzopangiwa na mkuu wake
    wa kazi.

✅AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES OFFICER II) – TGS.D

SIFA ZA KUINGILIA:-
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashada ya juu ya Ununuzi/Ugavi kutoka
katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali AU wenye “Professional level
III” inayotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini
(Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board – (PSPTB) au sifa nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na PSPTB, ambaye amesajiliwa na PSPTB kama “Graduate Procurement and Supplies Professional”.

KAZI ZA KUFANYA:-

  • Kutayarisha makisio ya vifaa vinavyohitajika (Schedule of
    Requirements).
  • Kuandaa utaratibu wa upokeaji wa vifaa
  • Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji na
    usambazaji wa vifaa.
  • Kusimamia upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa (Physical
    Distribution)
  • Kubuni mfumo wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location
    Index Design).
  • Kuandaa taarifa mbalimbali za vifaa.
  • Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kwa kufuata taratibu zilizopo.
  • Kuandaa hati za kupokelea vifaa.
  • Kutoa vifaa kwa watumiaji (Distribution goods to User department and other users).
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake atakzopangiwa na mkuu wake wa kazi.

✅AFISA UGAVI MSAIDIZI I (ASSISTANT SUPPLIES OFFICER I) – TGS C

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama July 06-2024

NAFASI za Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama July 06-2024

SIFA ZA KUINGILIA
Kuajiriwa wenye Stashahada ya Ununuzi/Ugavi au Biashara
iliyojiimarisha katika ununuzi na ugavi, kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali, au sifa inayolingana na hizo
inayotambuliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (Procurement and Supplies Professionals and Technician Board”.Awe amesajiriwa na PSPTB kama “Procurement and Supplies Full Technician” na awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

KAZI ZA KUFANYA

  • Kutunza na kupanga vifaa vilivyomo ghalani katika hali ya usafi na usalama.
  • Kupokea vifaa vilivyonunuliwa kutoka kwa wazabuni.
  • Kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.
  • Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kifaa kilichopo ghalani
  • Kufungua leja “Ledger” ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa
    vinavyoingia, kutunzwa na kutoka ghalani.
  • Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji kwa kuzingatia taratibu zilizopo.
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake
    wa kazi.

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – TGS C

SIFA ZA KUINGILIA:-
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada au NTA Level
6 katika mojawapo ya fani zifuatazo; Utunzaji wa kumbukumbu au Sheria
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kompyuta.

KAZI ZA KUFANYA:-
(a)Masjala za Kawaida

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista.
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista.
  • Kusambaza majalada kwa watendaji.
  • Kupokea majalada yanayorushwa masjala kutoka kwa watendaji.
  • Kurudisha majalada kwenye kabati la majalada.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ya Taasisi.

(b) Mahakama

  • Kupokea nyaraka au barua zinazohusu ufunguzi wa kesi za jinai na madai.
  • Kuandika samansi (summons) zinazohusu kesi za madai na jinai.
  • Kuandaa orodha ya kesi kila wiki na kutunza mafaili ya kesi
    zinazoendelea.

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II – TGS C

SIFA ZA KUINGILIA:-
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada (Diploma) ya
Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili. Aidha, wawe wamefaulu somo la
Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kup
ata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.

KAZI ZA KUFANYA:-

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu
    wanazoweza kushughulikiwa;
  • Kutunza taarifa, kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe
    za vikao safari za mkuu wake na ratiba ya kazi zingine;
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

✅DEREVA II – TGS B

SIFA ZA KUINGILIA:-

  • Waombaji wawe na cheti cha kidato cha nne (Form IV) na Leseni ya
    Daraja la E au C1 ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
  • Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari
    (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
  • Waombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II
    watafikiriwa kwanza.

KAZI ZA KUFANYA:-

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama
    wa gari,
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za
    kikazi,
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
  • Kufanya usafi wa gari, na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi
    wake.

✅MLINZI – TGOS A

SIFA ZA KUINGILIA:-
Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne, waliofuzu mafunzo ya
Mgambo au JKT na kupata cheti.

KAZI ZA KUFANYA:

  • Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje
    ya ofisi) ina hati ya idhini;
  • Kuhakikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake;
  • Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku;
  • Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi;
  • Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wanaidhini ya kufanya hivyo;
  • Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile moto, mafuriko n.k. na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile polisi na zimamoto;
  • Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.

✅MSAIDIZI WA OFISI – TGOS. A

SIFA ZA KUINGILIA;
Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne waliofaulu vizuri katika
masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.

KAZI ZA KUFANYA;

  • Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja
    na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani kupalilia
    bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na
    kusafisha vyoo;
  • Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofisa
    wanaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika;
  • Kusambaza barua za ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa;
  • Kutayarisha chai ya ofisi;
  • Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta;
  • Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinawekwa sehemu
    inayostahili;
  • Kufungua milango na madirisha ya ofisi wakati wa asubuhi na jioni
    kuyafunga baada ya saa za kazi;
  • Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia;
  • Kuweka majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi
    walizomo;
  • Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibik

MAELEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI WA KADA ZOTE.

  • Muombaji awe Raia wa Tanzania.
  • Maombi yote ya kazi yatumwe kwa njia ya kielektroniki kupitia tovuti ya Tume: www.jsc.go.tz (Nakala ngumu hazitapokelewa).
  • Barua ya maombi ya kazi iandikwe kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa
    Mahakama, S.L.P 8391, Dar es salaam.
  • Zingatia mambo yafuatayo wakati wa kujaza fomu ya maombi ya kazi:-
    ▪ Pakia kielektoniki (upload) vyeti vyote vya elimu na mafunzo pamoja na
    matokeo ya vyeti hivyo kadri utakavyohitajika kwenye fomu ya maombi;
    ▪ Pakia cheti cha kuzaliwa;
    ▪ Pakia picha ya rangi (passport size) ya hivi karibu kwenye fomu ya
    maombi;
    ▪ Taja namba za kitambulisho cha Taifa (NIDA);
    ▪ Pakia nyaraka nyingine kadiri fomu itakavyokuelekeza kutegemea na kazi.
  • Hizi ni nafasi za Ajira mpya kwa hiyo watumishi ambao tayari wana ajira za kudumu katika utumishi wa Umma hawastahili kuomba nafasi hizi;
  • Waombaji wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa lolote la jinai au kufungwa jela;
  • Waombaji watakaoshinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa
    Mahakama ya Tanzania na wawe tayari kupangiwa kwenye kituo chochote chenye nafasi wazi;
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na
    TCU/NACTE wakishindwa kutekeleza hili maombi yao hayatashughulikiwa;
  • Waombaji waliowahi kuachishwa/kufukuzwa kazi katika Utumishi wa Umma wasiombe;
  • Waombaji wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia masharti
    yaliyotajwa hapo juu maombi yao hayatashughulikiwa;
  • Waombaji watakaotoa taarifa za uongo mfano kuhusu umri wao, elimunyao au sehemu walizowahi kufanyia kazi na ikagundulika hata kama watakuwa wameshaajiriwa wataondolewa kazini ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
  • Waombaji wenye ulemavu watapewa kipaumbele.
  • Mwombaji abainishe aina ya ulemavu alionao kwenye barua ya maombi.
  • Kwa maelezo zaidi au msaada wasaliana kupitia simu ya maulizo:
    0734219821 na 0738 247341 au barua pepe: [email protected]

Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 20 Julai, 2024.

KUTUMA MAOMBI TAFADHALI BONYEZA HAPA

BONYEZA HAPA KUDONWLOAD PDF YA AJIRA ZA MAHAKAMA JULY 06-2024

Tags:

Comments are closed.