NAFASI za Kazi Tunduma Town Council August 06-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Kazi Tunduma Town Council August 06-2024
NAFASI za Kazi Tunduma Town Council August 06-2024, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Mji Tunduma kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye
Kumb Na. FA. 228/613/01/D/083 cha tarehe 25 Julai, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
✅DEREVA DARAJA II (DRIVER II) – (NAFASI 1)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; na
- Kufanya usafi wa gari
SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa mwenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni Daraja ‘E’ au ‘C’ ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali. Awe
amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo
cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGS B.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi waUmma; - Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili;
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa zakuingilia katika
kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi za kazi kwa Waajiri
wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato
cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua zakisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 19/08/2024.
Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Tunduma,
S.L.P. 73,
TUNDUMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemuiliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA
POST: DEREVA DARAJA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Mji ya Tunduma More Details |
2024-08-19 Login to Apply |