NAFASI za Kazi Wilaya ya Kilolo July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Kazi Wilaya ya Kilolo July 2024
NAFASI za Kazi Wilaya ya Kilolo July 2024,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya
kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na: FA.97/288/01”A”/2 cha tarehe 28 Mei, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III- NAFASI 4
MAJUKUMU YA KAZI
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa Amani na Msimamizi
wa Utawala Bora katika Kijiji; - Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji;
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa Taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika
kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali; - Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo; Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa
au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.
✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 3
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari “log book;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kufanya usafi wa Gari; na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), mwenye leseni Daraja ‘E’ au ‘C’ ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila
kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 4
KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye Regista (Incomming);
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register);
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers);
- Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji;
- Kutafuta kumbukumbu/ Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji;
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au
mahali Pengine yanapohifadhiwa; na - Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya utunzaji kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma. - Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa
Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards); - “Testmonial”, ‘‘Provisional Results”, “Statement of results”, hati ya matokeo ya Kidato
cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 12 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya Kilolo,
S.L.P. 2324,
KILOLO.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
POST: DEREVA DARAJA II – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo More Details |
2024-08-12 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo More Details |
2024-08-12 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 4 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo More Details |
2024-08-12 Login to Apply |