RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Wilaya ya Nyang’hwale 30-01-2024

Filed in Ajira, Michezo by on 30/01/2024

NAFASI za Kazi Wilaya ya Nyang’hwale 30-01-2024

NAFASI za Kazi Wilaya ya Nyang'hwale 30-01-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi ya Mkataba Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale 30-01-2024,Nafasi za kazi Chato, wilaya ya nyang'hwale, Ajira halmashauri ya nyang'hwale.

NAFASI za Kazi Wilaya ya Nyang’hwale 30-01-2024

NAFASI za Kazi Wilaya ya Nyang’hwale 30-01-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi ya Mkataba Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale 30-01-2024,Nafasi za kazi Chato, wilaya ya nyang’hwale, Ajira halmashauri ya nyang’hwale.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale kwa kuzingatia Kibali cha Ajira za Mkataba wa mwaka mmoja cha tarehe 02/01/2024 chenye Kumb.Na. FA.97/228/02″A”/113 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, anakaribisha maombi ya kazi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi zifuatazo.

1. Mhandisi II (Mitambo) (Nafasi 01) Ngazi ya Mshahara TGS E.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Kuajiriwa wenye shahada au stashahada ya juu ya uhandisi mitambo (Mechanical Engineering) kutoka vyuo Vikuu Vinavyotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU.

  • Kufanya ukaguzi wa ubora wa Magari na kurekebisha ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakiki viwango vya ubora wa vifaa vya matengenezo.
  • Kufanya usanifu na kusimamia utekelezaji wa miradi ya mitambo ya Halmashauri.
  • Kufanya kazi za matengenezo ya magari kwa kuzingatia taratibu zilizopo.
  • Kuandaa na kutunza kanzidata ya mitambo pamoja na matengenezo yake.
  • Kufuatilia maendeleo ya teknolojia mbalimbali ya ufundi kwa madhumuni ya kuboresha utaalamu wao kwenye fani ya ufundi.
  • Kufanya kazi utakazopangiwa na msimamizi wako wa kazi

2.Fundi sanifu II (Mitambo). (Nafasi 01) Ngazi ya Mshahara TGS C.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye stashahada ya mechanical Engineering kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuchunguza na kutambua matatizo ya Magari na mitambo ili kufanya matengenezo.
  • Kufanya matengenezo na ukaguzi wa mitambo chini ya usimamizi wa fundi sanifu mwandamizi.
  • Kufanya matengenezo kinga (Preventive maintainance) ya Clutch, Gearbox na mifumo ya breki.
  • Kufuatilia maendeleo ya teknolojia mbalimbali ya ufundi kwa madhumuni ya kuboresha utaalamu wake kwenye fani ya ufundi.
  • Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na msimamizi wako wa kazi.
NAFASI za Kazi Wilaya ya Nyang'hwale 30-01-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi ya Mkataba Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale 30-01-2024,Nafasi za kazi Chato, wilaya ya nyang'hwale, Ajira halmashauri ya nyang'hwale.

NAFASI za Kazi Wilaya ya Nyang’hwale 30-01-2024

3. Fundi sanifu Msaidizi (Mitambo). (Nafasi 01) Ngazi ya Mshahara TGS B.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne wenye Astashahada ya Mechanical Engineering kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kufanya matengenezo madogo na makubwa ya magari na mitambo.
  • Kuhakikisha usalama kwa watumishi na mali wakati wote wa utendaji kazi.
  • kuhifadhi na kutunza vifaa anavyofanyia kazi
  • Kuhakikisha vifaa vya karakana na mazingira yake ni safi wakati wote.
  • Kufanya uchunguzi, kubaini na kuandaa gharama za kurekebisha matatizo ya magari.
  • Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na msimamizi wako wa kazi.

4. Afisa Ugavi Msaidizi II (Nafasi 01) TGS C

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Kuajiriwa wenye Stashahada ya Ununuzi/ugavi kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali au sifa inayolingana na hizo na pia awe amesajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (Procurement and Supplies Professional Technician Board (PSPTB) kwa Ngazi ya Full Technician.
  • CHEZA Aviator Ushinde Mikeka ya Bure Kila Wiki

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kutunza na kupanga vifaa vilivyomo ghalani katika hali ya usafi na usalama.
  • Kupokea vifaa vilivyonunuliwa kutoka kwa wazabuni.
  • Kufungua na kutunza “Bin card” kwa kila kilichopo ghalani.
  • Kufungua leja (ledger) ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vilivyoingia, kutuzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.
  • Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine kwa kuzingatia taratibu zilizopo.
  • Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na usalama.
  • Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na msimamizi wako wa kazi.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
  • Waombaji wote waambatishe Picha mbili “Passport size “za hivi karibuni.
  • Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa, Kitambulisho cha Taifa (NIDA), kitambulisho cha mpiga kura au hati ya kusafiria.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji waambatanishe vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    i. -Degree/Advanced Diploma /Diploma/Certificates
    ii. -Cheti cha Mtihani wa kidato cha IV na VI
    iii. -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
    kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
    HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhiniwa na Mamlaka husika Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Baraza la Mitihani la Taifa, (NECTA) na Baraza la Elimu ya Ufundi Tanzania (NACTE)
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 11/02/2024, Muhimu, kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.

Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale,
S.L.P 352,
NYANG’HWALE

DOWNLOAD PDF CLICK HERE

Mkurugenzi wilaya chato, Shule za msingi wilaya ya nyang’hwale, Halmashauri ya wilaya ya Shule za msingi wilaya ya geita, Matokeo ya Shule za sekondari Mkoa wa Geita, Shule za msingi wilaya ya chato, Nida wilaya ya chato, Kata za halmashauri ya mji geita, NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA Geita 2024.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , , ,

Comments are closed.