NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Bukoba July 01-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Bukoba July 01-2024
NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Bukoba July 01-2024, Nafasi za Kazi za Madereva Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba July 01-2024.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA 01-07-2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kufuatia kupokea kibali cha ajira chenye kumb. Na. FA.228/613/01/C/059 cha tarehe 07.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimbenti ya Utumishi wa Utawala Bora anawatangiza watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini.
✅DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 1)
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV)
- Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Drivingi Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na
- Kufanya usafi wa gari.
NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni TGS B
MASHARTI YA UJUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
(referees) watatu wa kuaminika. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, Kidato
cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CCA. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 11 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA,
S.L.P 491,
BUKOBA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz// (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF
POST: DEREVA DARAJA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba More Details |
2024-07-14 Login to Apply |
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Nafasi za Kazi za Madereva Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba July 01-2024., NAFASI za Madereva Kutoka Wilaya ya Bukoba July 01-2024