NAFASI za Madereva Manispaa ya Moshi May 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Madereva Manispaa ya Moshi May 2024
NAFASI za Madereva Manispaa ya Moshi May 2024, Ajira za Madereva Manispaa ya Wilaya ya Moshi May 30-2024, Nafasi za Madereva Halmashauri ya Manispaa ya Moshi May 30-2024,TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI 30-05-2024.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA
.228/613/01/B/073 cha tarehe 02.04.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
DEREVA II- (NAFASI 1)
SIFA ZA MWOMBAJI
- Mwombaji awe na cheti cha kidato cha nne (form iv) na Leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
- Awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
KAZI NA MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (log book).
- Kufanya usafi wa gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.
MSHAHARA
Ngazi ya mshahara ni TGS B
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha
Nne, Kitado cha Sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Cheti cha Kompyuta, Vyeti vya kitaaluma (Professional Certificates from respective boards) “Testimonials”, Provisional Results”, “Statement of
results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI
RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na
NACTE). - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe. 12/06/2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya Elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa
Mkurugenzi Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa
S.L.P 318,
MOSHI-KILIMANJARO
Maombi yote yatumwe kwenye Mfumo wa kielectroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia Anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz// (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment
Portal’’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: DEREVA DARAJA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Manispaa ya Moshi More Details |
2024-06-12 Login to Apply |
BONYEZA HAPA DONWLOAD PDF
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Ajira za Madereva Manispaa ya Wilaya ya Moshi May 30-2024, Nafasi za Madereva Halmashauri ya Manispaa ya Moshi May 30-2024, NAFASI za Madereva Manispaa ya Moshi May 2024, TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI 30-05-2024.