NAFASI za Madereva Wilaya Ya Kibiti July 22-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Madereva Wilaya Ya Kibiti July 22-2024
NAFASI za Madereva Wilaya Ya Kibiti July 22-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, amepokea kibali cha Ajira Mpya
kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.
Hivyo anapenda kuwatangazia
Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada moja (01) kama ilivyoanishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –
✅DEREVA VIVUKO II (“Ferry/Boat Operator II”) NAFASI 02
KAZI NA MAJUKUMU
- Kufunga na kufungua kamba za mashua/kivuko.
- Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya mashua/kivuko
- Kupanga abiria au magari kwenye mashua/kivuko
- Kuendesha na kuongoza mashua/kivuko.
- Kutunza daftari za safari ya mashua/kivuko.
- Kuhakikisha kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.
- Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Waliohitimu Mtihani wa Kidato cha Nne, wenye ujuzi wa kuendesha na kutunza mashua / vivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulevu walionao kwa ajili ya
taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Provisional/ testimonial/ statement of Result na hati za matokeo za kidato cha Nne na
Sita (Form IV and Form Sixresults slip) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika Kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC.45/257/O1/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne, Kidato cha Sita kwa wale
waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa
za kazi husika. - Postgraduate/Deree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma (Proffesional Certificate from Respective Boards)
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Uwasilishaji wa taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
- Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 30 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 33,
KIBITI.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo:-https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA