NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu Wilaya ya Bukombe July 05-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu Wilaya ya Bukombe July 05-2024
NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu Wilaya ya Bukombe July 05-2024, Nafasi za Ajira za Msaidizi wa Kumbukumbu Kutoka Halmashauri Wilaya ya Bukombe July 05-2024, Ajira Mpya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe July 05-2024.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024.
Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma
maombi kwa kada Nafasi 4 za Msaidizi Wa Kumbukumbu II kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (“Records Management Assistant II”NAFASI 4)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliehitimu
mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Masijala kutoka
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa compyuta.
KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II.
- Kutafuta kumbukumbu /nyaraka/mafaili yanayohitajika
na wasomaji. - Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa Kumbukumbu/nyaraka.
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka
katika makundi kulingana na somo husika (Classification and
Boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi. - Kuweka/kupanga kumbukumbu /nyaraka katika reki (File Racks/Cabinets) katika masjala /vyumba vya kuhifadhia
kumbukumbu. - Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
- Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka Taasisi za Serikali. vii.Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
- NGAZI YA MSHAHARA:;Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS C1
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 nausiozidi miaka 45 isipo kuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavuwalionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Adress) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na
cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional
Certificate from Respective Boards). - Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18 Julai, 2024.
MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 02,
BUKOMBE.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa
ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani
hii pia inapaikana kwenye Tovuti ya Sekretariet ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe More Details |
2024-07-18 Login to Apply |
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Ajira Mpya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe July 05-2024., Nafasi za Ajira za Msaidizi wa Kumbukumbu Kutoka Halmashauri Wilaya ya Bukombe July 05-2024, NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu Wilaya ya Bukombe July 05-2024