RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu Wilaya ya Tandahimba July 05-2024

Filed in Ajira by on 05/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu Wilaya ya Tandahimba July 05-2024

NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu Wilaya ya Tandahimba July 05-2024, Ajira Mpya za Msaidizi wa Kumbukumbu Kutoka Halmashauri Wilaya ya Tandahimba July 05-2024, Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Leo July 05-2024.

NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu Wilaya ya Tandahimba July 05-2024

NAFASI za Msaidizi wa Kumbukumbu Wilaya ya Tandahimba July 05-2024, Ajira Mpya za Msaidizi wa Kumbukumbu Kutoka Halmashauri Wilaya ya Tandahimba July 05-2024, Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Leo July 05-2024.

Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kupitia kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA. 228/613/01/C/032 cha tarehe 21 Mei, 2024 na kibali cha ajira mpya chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 chenye Kada ya Msaidizi wa kumbukumbu Daraja la II nafasi tano (5) kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Hivyo Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya
Tandahimba anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa watanzania wote wenye sifa na kuleta maombi ya kazi kwa nafasi zilizoainishwa hapo chini,

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – NAFASI 5

SIFA ZA MWOMBAJI:

  • Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Masjala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

MAJUKUMU YA KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista
  • Kusambaza majalada kwa watendaji KupokeaKupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
  • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji
  • Kurudisha majalada kwenye Shubaka/kabati la majalada au mahali penginenyanapohifadhiwa
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS C1 kwa mwez

MASHARTI YA JUMLA YA MAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum
    Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu
    wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia
    sifa za kazi husika.
    Postgraduate/Degree/Advanced
    Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo yabKidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
    HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18/07/2024

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji (W),
S.L.P O3,
TANDAHIMBA – MTWARA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira kupitia anwani
ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , ,

Comments are closed.