RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024

Filed in Ajira by on 04/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024

NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024, Ajira za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu Leo July 04-2024, Nafasi za Kazi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu 04-07-2024.

NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024

NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024, Ajira za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu Leo July 04-2024, Nafasi za Kazi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu 04-07-2024.

Kwa mujibu wa kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu anawatangazia wananchi wote Raia wa Tanzania kuomba nafasi za Kazi zifuatazo:-

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (NAFASI – 1)

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha nne au sita mwenye Stashahada (Diploma) ya
Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la
Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata
program za Kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, powerpoint, internet, Email
na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI II

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
  • Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu
    wanapoweza kushughulikiwa.
  • Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, mihadi, wageni, tarehe ya
    vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi za kazi nyingine zilizopangwa kutekelezwa katika Ofisi anayofanyia kazi, kumtarifu mkuu wake kwa wakati
    unaohitajika.
  • Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
  • Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
  • Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maafisa walio katika sehemu alipo na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B

MASHARTI YA JUMLA

  • Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya Miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
  • Mwombaji aambatishe nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika pamoja na namba zao za Simu.
  • Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya Elimu na taaluma kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, na vilivyothibitishwa na Wakili au
    Kamishna wa Viapo.
  • Testimonials, provision results, statement of results, havitakubaliwa
  • Waombaji wote ambao wamesoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao
    vinafanyiwa ulinganishi na TCU na NACTE.
  • Waomabji waambatanishe picha moja passport size ya hivi karibuni
  • Barua ya Maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kingereza

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17 Julai, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 1288,
KISHAPU.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kieletroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ anuani
hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Secretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa “Recruitment Portal”

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , ,

Comments are closed.