RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Kwimba June 22-2024

Filed in Ajira by on 22/06/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Kwimba June 22-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Kwimba June 22-2024, Ajira Mpya za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Leo Juni 22-2024, Ajira Mpya za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba 22-06-2024.

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Kwimba June 22-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Kwimba June 22-2024, Ajira Mpya za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Leo Juni 22-2024, Ajira Mpya za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba 22-06-2024.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KWIMBA 22-06-2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba amepokea Kibali cha Ajira Mbadala kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Barua yenye Kumb. Na. FA.228/613/01/C/028 ya tarehe 20 Juni,
2024.Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI (4)

SIFA ZA KUAJIRIWA
Waombaji wanatakiwa wawe wenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form Six) aliyehitimu astashahada/ cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi yabSanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI.

  • Afisa Masuuli na Mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
  • Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalama katika kijiji;
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
  • Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.
  • Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wake

MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wawasilishe maelezo binafsi (Curriculum Vitae) yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye Anuani na Namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika.
  • Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Sita, Taaluma na cheti cha kuzaliwa.
  • Waombaji watakaowasilisha” Result Slip”,”bStatement of Results”,” Provisional Results ”au” Transcripts HAVITAKUBALIKA.
  • Kwa Waombaji waliosoma nje ya Nchi, Elimu ya Kidato cha Nne au Sita wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
  • Kwa waombaji waliosoma Vyuo nje ya Nchi wawasilishe uthibitisho kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
  • Waombaji watakokidhi sifa zinazotakiwa ndio watakaoitwa katika usaili.
  • Barua ya maombi iliyosainiwa na Mwombaji inaweza kuandikwa kwa lugha yabKiingereza au Kiswahili.
  • Waombaji wenye mahitaji maalum (special needs/disability) wanatakiwabkuainisha kwenye maombi yao.
  • Waombaji watakaowasilisha Taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuombabisipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 05 Julai, 2024

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika
tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , ,

Comments are closed.