KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Nachingwea May 2024 

Filed in Ajira by on 31/05/2024 0 Comments

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Nachingwea May 2024

NAFASI za Mtendaji wa Vijiji Wilaya ya Nachingwea May 2024, Nafasi za Mtendaji wa Kijiji Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea May 30-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea May 30-2024, Nafasi Mpya za Kazi za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea May 2024,TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA 30-05-2024.

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Nachingwea May 2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Nachingwea May 2024 , Nafasi za Mtendaji wa Kijiji Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea May 30-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea May 30-2024, Nafasi Mpya za Kazi za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea May 2024,TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA 30-05-2024.

Kwa kuzingatia kibali cha ajira Kumb.Na. FA.228/613/01/B/065 cha tarehe 15 Machi, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu ajira mbadala.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea anatangaza nafasi za kazi na kukaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa kujaza nafasi kama zilivyoorodheshwa katika tangazo hili :-

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI MOJA (1)

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha nne/sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) Katika moja wapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, usimamiziwa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo,D odoma au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI

 • Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
 • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao,kuwa mlinzi wa amani na msimamizi
  wa utawala bora katika kijiji.
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Mendeleo ya kijiji.
 • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya kijiji.
 • Kutafsiri na kusimamia sera,sheria na taratibu.
 • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
 • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika kijiji.
 • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
 • Mwenyekiti wa kikao cha wataalaamu waliopo katika kijiji
 • Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
 • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji na atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
 • Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali TGS B

MASHARTI KWA JUMLA

 • Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu
  ya Miaka 18.
 • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
 • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe (E- mail address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
 • “Provisional/Testimonials/Statement of results” na hati za matokeo za kidato chabnne na sita (form IV na VI result slip) HAVITAKUBALIWA.
 • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
 • Wombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
 • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika
  kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri
  wao na waajiri wao wajiridhishe iapasavyo.
 • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na Wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyokatika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
 • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbali mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
 • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA)
 • Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
 • Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Ijumaa, tarehe 12 JUNI, 2024.

MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

MKURUGENZI MTENDAJI (W),
1 BARABARA,
BOMANI-MATANGINI,
S. L. P 291,
65335 BOMA, NACHINGWEA

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https:portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *