NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Ngorongoro May 24-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Ngorongoro May 24-2024
NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Ngorongoro May 24-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro May 24-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Leo May 24-2024, Nafasi za Watendaji wa Vijiji May 2024.
- NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Chamwino May 24-2024
- MAJINA ya Walioitwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT 2024
POST MTENDAJI WA KIJIJI III – 1 POST
EMPLOYER Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
APPLICATION TIMELINE: 2024-05-24 2024-06-12
JOB SUMMARY NIL
MAJUKUMU YA KAZI
- Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji;
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
- Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
- Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya klitaalam katika kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya kidato cha Nne(IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo:
Utawala,Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro More Details |
2024-06-12 Login to Apply |
Historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Chimbuko la eneo
Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro ni mojawapo kati ya Halmashauri za Wilaya sita na Jiji moja zilizopo katika Mkoa wa Arusha Nchini Tanzania.
Makao Makuu ya Wilaya yapo Loliondo Wasso umbali wa takriban kilomita 400 kutoka Makao Makuu ya Mkoa.
Wilaya hii ilianzishwa mwaka 1979 chini ya sheria namba 5 ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Mwaka 1982 ikiwa na Tarafa tatu za Loliondo, Sale na Ngorongoro.
Tarafa ya Ngorongoro imo kwenye eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) iliyoanzishwa kwa Sheria Sura 413 ya mwaka1959 (NCA, CAP 284 (R.E.2002) na linasimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
Utawala na watu wake
Wilaya ya Ngorongoro inapakana na Nchi jirani ya Kenya kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Serengeti kwa upande wa Magharibi, Wilaya za Monduli na Longido kwa upande wa Mashariki na Wilaya ya Karatu kwa upande wa Kusini.
Kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Wilaya ya Ngorongoro ilikuwa na idadi ya watu 174,278 Wanaume wakiwa ni 82,610 na Wanawake ni 91,668 ambapo wastani wa ukubwa wa kaya ni 4.8 na ongezeko la watu katika Mkoa wa Arusha ‘growth rate’ ikiwa ni asilimia 2.9~3.
Ukubwa wa Eneo
Wilaya ya Ngorongoro ina eneo la kilometa za mraba zipatazo 14,036 ambalo lipo katika nyuzi 30030’ kusini mwa Ikweta na 35042’ Mashariki mwa Greenwich na urefu wa mita 1,009 hadi 3,645 kutoka usawa wa bahari.
Mgawanyo wa ardhi katika Wilaya ya Ngorongoro ni kama ifuatavyo:-
- Eneo la kwanza ni eneo lililopo chini ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro lenye ukubwa wa kilometa za mraba 8,292 sawa na asilimia 59 za eneo lote la Wilaya. Eneo hili la Hifadhi hutumika kwa malisho ya mifugo na Wanyamapori na pia shughuli za kitalii.
- Eneo la pili ni pori Tengefu la Loliondo linalojumuisha Tarafa yote ya Loliondo na sehemu ya Tarafa ya Sale lenye ukubwa wa kilometa za mraba 4,000 sawa na asilimia 28.4. Eneo hili hutumika kwa shughuli za Kilimo, Ufugaji, Hifadhi ya wanyama, Misitu, Biashara, utalii na makazi.
- Eneo la tatu ni eneo la pori tengefu la ziwa Natron linalojumuisha sehemu iliyobaki ya Tarafa ya Sale lenye ukubwa wa kilometa za mraba 1,744 sawa na asilimia 12.4
Hali ya hewa
Kwa ujumla Wilaya ya Ngorongoro ina maeneo ya joto la washastani hasa katika Tarafa ya Sale na hali ya Kitropikali Wilaya Ngorongoro ina mvua za wastani wa 800mm hadi 1,000mm na upepo Mkali unaovuma kutoka Mashariki kuelekea Magharibi. Maeneo makubwa ya Wilaya ya uoto wa asili jamii ya Akashia hasa ukana wa Kati, Mashariki na Magharibi. Upande wa Mashariki na Magharibi kuna Ukanda wa bonde la Ufa na misitu Mkubwa. Upande wa Kusini mwa Wilaya ni eneo maarufu la Hifadhi ya Ngorongoro linalochukua asilimia 59 ya wilaya ambalo lipo katika Tarafa moja ya Ngorongoro.
Katika wilaya hii ndipo lilipo bonde la Ngorongoro maarufu kama Ngorongoro kreta na mlima Ol-Doinyo Lengai ambapo ni aina ya milima volcano hai. Kutokana na Jiographia ya eneo na hali ya hewa sehemu ya wilaya ya Ngorongoro ndiyo kitovu cha mapitio ya nyumbu na mazalia yake hasa ikiwa sehemu ya ecolojia ya Serengeti.
Uoto wa Asili
Wilaya ina misitu minne (4) ya asili iliyosajiliwa ambayo ni:-
- Msitu wa Loliondo I unaosimamiwa na Halmashauri ya Wilaya.
- Msitu wa Loliondo II unaosimamiwa na jamii msitu huu upo katika kata ya Enguserosambu
- Msitu wa Jamii wa Sariani unaosimamiwa na jamii ya vijiji vitano
- Msitu wa nyanda za Juu Ngorongoro “Ngorongoro Highlind Forest” unaosimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Ajira za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro May 24-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Leo May 24-2024, Nafasi za Watendaji wa Vijiji May 2024., NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Ngorongoro May 24-2024