RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Pangani June 06-2024

Filed in Ajira by on 06/06/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Pangani June 06-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Pangani June 06-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Leo June 06-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Halmashauri Mbalimbali Tanzania, Nafasi za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Pangani June 2024.

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Pangani June 06-2024

NAFASI za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Pangani June 06-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Leo June 06-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Halmashauri Mbalimbali Tanzania, Nafasi za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Pangani June 2024.

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI 06-06-2024

Kwa kuzingatia Kibali cha ajira Kumb. Na. FA.228/613/01/C/023 cha tarehe 20 Mei, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu ajira Mbadala.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani anatangaza nafasi ya Kazi na kukaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa kujaza nafasi kama zilivyoorodheshwa katika tangazo hili: –

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI MOJA (1)

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Kuajiriwa mwenye elimu ya
    Kidato cha nne/sita aliyehitimu
    mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) Katika moja wapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI

  • Afisa Masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
  • Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa Utawala bora katika Kijiji
    TH.
  • Kuratibu na Kusimamia upangaji wa Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji
  • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, Umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
  • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
  • Kusimamia, Kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
  • Mwenyekiti wa kikao cha Wataalam waliopo katika Kijiji
  • Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya Wananchi
  • Kusimamia Utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji na
  • Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Mishahara ya Serikali TGS B

MASHARTI KWA JUMLA

  • Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya Simu na Anuani ya barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • “Provisional/Testimonials/Statement of results” na hati za matokeo za Kidato cha nne na sita (form IV na VI result slip) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika Kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waoombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyokatika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA)
  • Uwasilishaji wa Taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.
  • Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahiili au Kingereza.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Jumatano, tarehe 19 Juni, 2024

MUHIMU kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa
MKURUGENZI MTENDAJI (W), Halmashauri ya Wilaya ya Pangani
S.L.P 89,
PANGANI.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

SHARE THIS POST:

Tags: , , ,

Comments are closed.