KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

NAMNA Bora ya Kuandika Barua ya Kuomba Kazi

Filed in Ajira, Makala by on 04/06/2024 0 Comments

NAMNA Bora ya Kuandika Barua ya Kuomba Kazi

NAMNA Bora ya Kuandika Barua ya Kuomba Kazi

NAMNA Bora ya Kuandika Barua ya Kuomba Kazi

NAMNA Bora ya Kuandika Barua ya Kuomba Kazi,Jifunze hapa namna borq ya kuandika barua nzuri ya kuomba ajira (kazi), mbinu za kuandika barua za kuomba kazi (ajira) namna ya kuandaa CV nzuri ya kuombea Kazi.

JE NI IPI BARUA YA KUOMBA KAZI?

NI TOFAUTI NA BARUA NYINGINE?

Barua ya kuomba kazi ni tofauti na Barua nyingine.

Barua ya kuomba kazi ina madhumuni ya kukutambulisha kwa mwajiri mtarajiwa.

Hii ni nafasi adhimu ambayo inabidi itumiwe vizuri.

Taarifa zote zinazokuhusu wewe ni muhimu zikawepo katika barua hii ili kuweza kumshawishi mwajiri mtarajiwa.

Hakikisha unaweka ujuzi, taaluma na uzoefu ulionao ambao utakufanya wewe kuwa mtahiniwa unayehitajika kujaza nafasi iliyopo.

Hizi ndizo taarifa ambazo Waajiri huangalia wanaposoma barua yako ya kuombea Kazi.

Unajua kwanini unatakiwa kuambatanisha barua pamoja na CV wakati wa kuomba kazi?

Barua hii huwekwa kwa madhumuni ya kujitambulisha kwa mwajiri mtarajiwa kwa kuzingatia nafasi uiombayo.

NAMNA Bora ya Kuandika Barua ya Kuomba Kazi

Kwa kawaida taarifa unazoziweka katika barua hii huwa ni kama kujitangaza mwenyewe na sifa zako na kwa namna gani sifa na ujuzi ulionao utakusaidia katika kufanya kazi unayoiomba.

Barua hii ikiandikwa vizuri humpelekea mwajiri kupitia CV yako kama hatua nyingine.

Je ni wakati gani na ni wapi utume barua yako?

Barua hii huitajika pale ambapo nafasi ya kazi huwa imetangazwa.

Hata kama tangazo la kazi halijakutaka uandike barua hii, siku zote ni vizuri na huongeza uzito kama itaambatanishwa na CV.

Barua hii ni tangazo kuhusu wewe, ni vizuri ukaiandika katika namna ambayo itakuuza vizuri katika soko la ajira.

Vile vile unaweza kutuma barua ya kuomba kazi isiyokuwa mahsusi kama mawakala wa kuajiri (recruitment agent) hawajatangaza kazi.

Katika hali kama hii jitahidi barua yako iwe na taarifa zote muhimu ambazo zitakusaidia kupata kazi.

Ni kama unatuma barua katika jopo la waajiri ambao kila mmojawapo ana vitu vyake anavyovipenda hivyo ni vizuri ukajielezea kiundani zaidi ili kuwapa fursa ya kukuona wewe katika muonekanao tofauti tofauti.

Kila barua ni vizuri ikaandikwa kwa kuzingatia mahitajai ya kazi iombwayo.

Je unaweza kuomba kazi bila kuona tangazo la kazi?

Wakati mwingine unaweza kuamua kuandika barua ya kuomba kazi katika kampuni fulani hata kama hawajatangaza kazi.

Kitu cha muhimu ni kuandika barua hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya mwajiri unayemlenga.

Uandishi wa barua hii ni tofauti huanza kwa kufanya tafiti iliyojitosheleza katika kampuni unayoilenga.

Lengo likiwa ni kufahamu majukumu, itikadi na malengo ya kampuni husika ambayo yatakusaidia wewe kuandika barua yenye mvuto na inayoendana na mahitaji ya kampuni.

Vile vile barua yako ni vizuri ikaomba kukutana na mwajiri kwaajili ya majadiliano zaidi, kama vile kuombwa kuitwa kwenye usahili.

Hakikisha mara zote unaonyesha ujuzi na utaalamu unaohitajika, mwajiri hatokuchagua wewe dhidi ya wengine wengi kwasababu ya kiingereza chako kizuri, uzuri wako lakini atakuchagua kwa sababu ya ujuzi ulionao unaohitajika katika kazi husika.

Ni muhimu kuhakikisha kuwa kila unapokutana na mwajiri mtarajiwa unaonyesha ujuzi na utaalamu ulionao ili kukurahisishia kupata kazi.

Je ni ipi njia muafaka ya kutuma barua yako?

Kwa kuzingatia maendeleo ya teknolojia, mfumo wa barua pepe ni njia muafaka na nafuu zaidi kutuma barua hizi.

Hakikisha unafuata mahitaji yote muhimu ya kuandika barua maalumu wakati wa kuandika barua ya kuomba kazi.

Vile vile hakikisha kuwa ujuzi na uzoefu wote uliouweka katika barua yako pia upo katika CV yako ambayo utaiambatanisha na barua hiyo.

Ukitekeleza haya utakuwa na nafasi kubwa ya kuitwa kwenye usahili.

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *