NATHAN Fasika Idumba atajwa Simba
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NATHAN Fasika Idumba atajwa Simba
NATHAN Fasika Idumba atajwa Simba, Klabu ya Simba imefanya mazungumzo na wawakilishi wa mlinzi wa kimataifa wa Congo DR Nathan Fasika Idumba mwenye umri wa miaka 25.
Fasika ambaye kwa sasa anaitumikia Valerenga ya Norway kwa mkopo akitokea Cape town City ya Afrika Kusini, sio mara ya kwanza Simba kujaribu kumsajili mchezaji huyo.
Simba ilitajwa kumwania Fasika msimu uliopita wa 2023/2024 kabla ya Valerenga kufanikiwa kumsajili kwa mkopo.
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali, baada ya kufanikisha usajili wa Lameck Lawi kutoka Coastal Union, alisema kuwa kuna usajili mwingine wa beki wa Kimataifa ambao wataukamilisha siku chache zijazo.
Wiki ijayo itakuwa busy kwa Simba kwani ndio wiki ya kukamilisha michakato yote ya usajili kabla ya kikosi kuelekea Misri kwaajili ya Pre-season.