RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA

INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA

INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA

AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA

NDEJEMBI Ataka Kukamatwa Waganga Wapiga Ramli Chonganishi

Filed in Habari by on 09/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NDEJEMBI Ataka Kukamatwa Waganga Wapiga Ramli Chonganishi

Na Mariam Kagenda – Kagera

Waziri Ndejembi akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera wakati wa uzinduzi wa kampeini ya Kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino

Waziri Ndejembi akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera wakati wa uzinduzi wa kampeini ya Kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino

Wakuu wa Mikoa nchini wameagizwa kufanya operesheni ya kukamata waganga wa tiba asili na tiba mbadala wasio na leseni ambao wanajihusisha na ramli chonganishi zinazochangia vitendo vya kikatili dhidi ya Watu wenye Ualbino.

Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi leo Julai 9, 2024 Mkoani Kagera wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya watu Wenye Ualbino iliyozinduliwa katika kata ya Kamachumu mkoani Kagera ambayo imeambatana na kauli mbiu isemayo “Mimi nipo ninapinga ukatili dhidi ya watu Wenye Ualbino”

Watoto wenye Ualbino wakiimba shairi wakati wa Uzinduzi wa Kampeini ya kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye Ualbino

Watoto wenye Ualbino wakiimba shairi wakati wa Uzinduzi wa Kampeini ya kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye Ualbino

Vile vile, Mhe. Ndejembi amewataka Wakuu hao wa Mikoa kuhakikisha wanafanya kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino katika Halmashauri zote na kuhakikisha kamati za watu wenye ulemavu zinaimarishwa katika maeneo yao kwani ni takwa la kisheria kupitia sheria namba 19 ya mwaka 2010 ya watu Wenye Ulemavu.

Mhe. Ndejembi Pia ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Mabalozi wa ulinzi wa Mtu Mwenye Ualbino kwa kutoa elimu, kupinga ukatili na kutoa taarifa kwa viongzo pale wanaposikia ama kuona viashiria vya ukatili dhidi ya watu hao.

Waziri wa nchi,Ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu akitoa pole kwa mama mzazi wa Asimwe Novath

Waziri wa nchi,Ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu akitoa pole kwa mama mzazi wa Asimwe Novath

Uzinduzi huo umefanyika ikiwa ni siku chache tangu mtoto Asimwe Novath mwenye umri wa miaka 2 na nusu mwenye Ualbino kuuwawa kisha mwili wake kutupwa kwenye Karavati

Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeini ya kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino

Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeini ya kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa amesema ataendelea kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kuhakikisha vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino vinakomeshwa Mkoani humo.

Makamu Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino Tanzania Alfred Kapole akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera wakati wa uzinduzi wa Kampeini ya Kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania Alfred Kapole ameishukuru serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia kundi la Watu Wenye Ualbino ikiwa ni pamoja na kuwasaidia vifaa kinga.

Wananchi wa mkoa wa Kagera walioudhuria uzinduzi wa Kampeini ya Kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino

Wananchi wa mkoa wa Kagera walioudhuria uzinduzi wa Kampeini ya Kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.