NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Tabora Mjini July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Tabora Mjini July 2024
NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Tabora Mjini July 2024, Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Tabora Mjini July 2024, Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Tabora Mjini, Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC Halmashauri ya Manispaa ya Tabora July 2024.
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI ZA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BVR KIT
- NEC Yaanzisha Mfumo wa Kupata Kitambulisho Online OVRS
- MASWALI Yanayoulizwa Mara Kwa Mara Ajira za INEC
Afisa mwandikishaji Jimbo la Tabora Mjini anapenda kuwajulisha kuwa, wafuatao wameitwa kwenye usaili wa nafasi za waandishi wasaidizi na Waendesha Vifaa vya BVR KIT (OPERATOR) katika zoezi la Uboresahji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakaofanyika kwa siku Mbili katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuanzia Tarehe 11.07.2024 hadi 12.07.2024 kama inavyoeleza hapa chini:-
KUNDI A
Kata za: Ikomwa, Kakola, Uyui, Kabila, Misha, Kalunde, Tumbi, Ntalikwa, Kanyenye, Malolo, Mwinyi, Itetemia, Kitete, Ng’ambo na Tambukareli.
Waombaji kutoka kata tajwa hapo juu wanatakiwa kufika Tarehe 11.07.2024 saa 2:00 asubuhi katika Ukumbi wa Halamashauri ya Manispaa Tabora kwaajili ya Usaili.
KUNDI B
Itonjanda, Ifucha, Ndevelwa, Mbugani, Gongoni, Kiloleni, Mapambano, Cheyo, Ipuli, Mpela, Mtendeni, K/Chekundu, Chemchem na Isevya.
Waombaji kutoka kata tajwa hapo juu wanatakiwa kufika Tarehe 12.07.2024 saa 2:00 asubuhi katika Ukumbi wa Halamashauri ya Manispaa Tabora kwa ajili ya Usaili.
NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Tabora Mjini July 2024
DONWLOAD PDF YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI NEC JIMBO LA TABORA MJINI JULY 2024
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema watu wote wenye sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wataandikishwa hata kama hawana kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bi. Giveness Aswile tarehe 15 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Tume na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri.
Mkutano huo unahitimisha mfululizo wa mikutano ambayo Tume imefanya na wadau wake kauanzia tarehe 07 Juni, 2024. Baadae Tume itafanya mikutano na wadau kwenye mikoa yote kwa kuzingatia ratiba ya uboreshaji wa Daftari.
Mikutano hiyo ina lengo Ia kuwapa wadau taarifa za uwepo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari Ia Kudumu la Wapiga Kura na kuwapitisha katika vifaa na mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni.
“Kuwa na kadi ya NIDA sio kigezo cha kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu Ia Wapiga Kura. Wananchi wote wenye sifa wataandikishwa bila kujali kama wana kadi ya NIDA au la,” amesema Bi. Aswile.
Ameyataja mambo yatakayohusika kwenye uboreshaji wa daftari kuwa ni pamoja na kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu 2025 na kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walioandikishwa awali.
Mambo mengine ni kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania au kifo.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Tabora Mjini, Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC Halmashauri ya Manispaa ya Tabora July 2024., Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Tabora Mjini July 2024, NEC Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Tabora Mjini July 2024