NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nzega Vijijini July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nzega Vijijini July 2024
NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nzega Vijijini July 2024, Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Nzega Vijijini July 08-2024, Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Nzega, Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC Jimbo la Nzega Halmashauri ya Wilaya ya Nzega July 08-2024.
ORODHA YA MAJINA WAIOITWA KWENYE USAILI JIMBO LA NZEGA VIJIJINI KWA WALIOMBA KAZI ZA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHAJI WA VIFAA VYA BAYOMETRIKI HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Nzega Vijijini Anawatangazia Waombaji wa Kazi za Waandishi Wasaidizi na waendeshaji vifaa vya bayometriki kupitia jimbo la nzega vijijini wanaitwa kwenye usaili utakaofanyika tarehe 12/07/2024 ofisi ya makao makuu ya halmashauri ya wilaya nzega-lubisu kuanzia saa 1:30 asubuhi.
waombaji wote mnatakiwa kufika na vyeti halisi vya kitaaluma, cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha nida au mpiga kura au leseni ya udereva au hati ya kusafiria.
WALIOITWA KUFANYA USAILI JIMBO LA NZEGA VIJIJINI-NZEGA DC PDF
NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nzega Vijijini July 2024
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema watu wote wenye sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wataandikishwa hata kama hawana kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bi. Giveness Aswile tarehe 15 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Tume na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri.
Mkutano huo unahitimisha mfululizo wa mikutano ambayo Tume imefanya na wadau wake kauanzia tarehe 07 Juni, 2024. Baadae Tume itafanya mikutano na wadau kwenye mikoa yote kwa kuzingatia ratiba ya uboreshaji wa Daftari.
Mikutano hiyo ina lengo Ia kuwapa wadau taarifa za uwepo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari Ia Kudumu la Wapiga Kura na kuwapitisha katika vifaa na mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni.
“Kuwa na kadi ya NIDA sio kigezo cha kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu Ia Wapiga Kura. Wananchi wote wenye sifa wataandikishwa bila kujali kama wana kadi ya NIDA au la,” amesema Bi. Aswile.
Ameyataja mambo yatakayohusika kwenye uboreshaji wa daftari kuwa ni pamoja na kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu 2025 na kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walioandikishwa awali.
Mambo mengine ni kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania au kifo.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Majina Mapya ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Nzega, Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili NEC Jimbo la Nzega Halmashauri ya Wilaya ya Nzega July 08-2024., Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC Jimbo la Nzega Vijijini July 08-2024, NEC Walioitwa Kwenye Usaili Jimbo la Nzega Vijijini July 2024