NECTA Yafuta Maswali ya Kuchagua Mtihani wa Hisabati
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NECTA Yafuta Maswali ya Kuchagua Mtihani wa Hisabati
NECTA Yafuta Maswali ya Kuchagua Mtihani wa Hisabati,Serikali inazidi kufanyia kazi maoni ya wadau wa Elimu kwa lengo la kuboresha mfumo wa Elimu nchini, ni baada ya kutangaza kuachana na mfumo wa kutahini somo la hisabati katika mtihani wa kumaliza darasa la saba, kwa kutumia utaratibu wa maswali ya kuchagua.
Akizungumza jijini Tanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania, (NECTA) Dk Said Mohamed amesema kuwa mtihani wa Hisabati kwa Shule za Msingi hautakuwa na maswali ya kuchagua kama ilivyozoeleka kwa miaka ya nyuma.
Amesema kuwa Mafunzo Mbalimbali yamekuwa yakiendelea kwa wadau husika na Mafunzo yanaendelea,lengo likiwa ni kuboresha ufaulu,hivyo utaratibu huo kwa baadae utafanyika hata kwa baadhi ya masomo ya Sekondari.
Ametaja Masomo ambayo baadaee yanatarajiwa kuachana na Mfumo wa Maswali ya kuchagua ni Biolojia, Kiingereza na Fizikia.
‘’Yote yanaendelea kufanyiwa tathmini ya kubadilishwa mfumo wake wa mtihani kama somo la hisabati,’’ amesema.
Necta ilibadili Mfumo wa kutahini hisabati kutoka ule wa kukotoa hadi wa maswali ya kuchagua mwaka 2018,hatua iliyozua mjadala mzito wa Kitaifa.
Wadau wakikosoa mfumo huo mpya wakisema ulikuwa ukitoa fursa kwa watahiniwa kubahatisha na kupatia majibu, na hivyo hata wasiokuwa na uwezo waliweza kufaulu na kuendelea na Masomo ya Sekondari.