NEW Amaan Complex Ruksa Kutumika Ligi Kuu 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NEW Amaan Complex Ruksa Kutumika Ligi Kuu 2024/2025
NEW Amaan Complex Ruksa Kutumika Ligi Kuu 2024/2025,Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Almas Kasongo amesema kuwa kuanzia msimu ujao wa Ligi 2024/2025 ni ruksa kwa timu ya Ligi Kuu Bara kutumia viwanja vya Zanzibar.
Kasongo ameyasema hayo mbele ya wanahabari kwenye semina iliyoandaliwa na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB).
Kasongo alisema kuwa katika kanuni iliyofanyiwa maboresho kuelekea msimu mpya ruhusa ya viwanja vya Zanzibar kutumika na timu za Ligi Kuu Bara ni kanuni moja wapo iliyofanyiwa marekebisho.
NEW Amaan Complex Ruksa Kutumika Ligi Kuu 2024/2025
“Katikati ya msimu ofisi yangu illipokea ombi la timu ya Simba kwenda kutumia uwanja wa New Amaan Complex kwaajili ya Ligi Kuu, lakini haikuwezekana kwa sababu ya kanuni japo hoja zao zilikuwa na mashiko.
“Tulikaa na Kamati ya Utendaji ya TFF na tukaona hakuna sababu ya kuzuia hilo na tukaona ni vyema kanuni hiyo ianze kutumika msimu ujao 2024/25,” alisema Kasongo.
Wakati huo huo, Kasongo amesema ndani ya siku mbili umma utafahamu ratiba na maboresho ya Ligi Kuu Bara 2024/2025.