Ni Simba vs Al Ahly Tripoli Kombe la Shirikisho 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uhamiaji katika mchezo wa pili wa hatua ya awali Kombe la Shirikisho la CAF uliopigwa nchini Libya jana, klabu ya Al Ahly Tripoli imefuzu raundi ya kwanza na sasa itacheza na Simba katika mchezo wa mtoano kuwania Kufuzu Makundi.
Soma na hii: Simba Queens vs Kenya Police Bullets Nusu Fainali CECAFA
Wafahamu wapinzani wa Simba SC Kombe la Shirikisho raundi ya Kwanza 2024/2025.
Al Ahly Tripoli imefuzu hatua hiyo ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, mchezo wa kwanza wakishinda mabao 2-0 na mabao 3-1 kwenye mchezo wa pili, huku mechi zote mbili zikipigwa chini Libya.
Katika raundi hiyo ya Kwanza Klabu ya Simba itaanzia ugenini nchini Libya na kumalizia nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.
Al Ahly Tripoli wapinzani wa Simba SC Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025
Michezo ya kwanza ya raundi hiyo inatarajiwa kuchezwa kati ya 13-15 September, huku marudiano itakuwa kati ya 20-22 September 2024.
Mshindi wa matokeo ya jumla kati ya Simba Sc na Al Ahli Tripoli atajikatia tiketi ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup 2024/25)