NICKSON Clement Kibabage Asaini Mkataba Mpya
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NICKSON Clement Kibabage Asaini Mkataba Mpya
NICKSON Clement Kibabage Asaini Mkataba Mpya,Beki wa kushoto Nickson Clement Kibabage ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia Young Africans SC.
Maamuzi hayo yamefikiwa na Yanga ikiwa ni katika kuendelea kuboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao wa 2024/2025.
Kibabage ambaye amekuwa na uwezo wa kuzuia na kupandisha mashambulizi kutokea upande wa kushoto, alijiunga na Young Africans SC mwanzoni mwa msimu wa 2023/2024.
Akiwa ndani ya Young Africans ambapo amecheza kwa msimu mmoja, amebeba ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Bank Federation, huku pia akiwemo katika mafanikio ya timu iliyocheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/2024.
Nickson Kibabage amekuwa na mchango mkubwa kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu NBC msimu uliopita wa 2023/2024 na ukiwa msimu wake wa kwanza alimaliza akiwa na “assist” tano.
Katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa, uongozi wa Yanga unaendelea kuboresha kikosi kwa kusajili wachezaji wapya na kuwaongezea mikataba wale ambao benchi la ufundi likiongozwa na Miguel Gamondi limependekeza waendelee kuwepo.