NIT Mafunzo ya Udereva wa Magari ya Mizigo HGV
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NIT Mafunzo ya Udereva wa Magari ya Mizigo HGV
NIT Mafunzo ya Udereva wa Magari ya Mizigo HGV, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kupitia kituo chake cha Umahiri cha Kikanda katika Usalama Barabarani (Regional Centre of Excellence for Road Safety) kitashiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yenye kaulimbiu “Endesha Salama Ufike Salama” yatakayofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 26 Agosti hadi 01 Septemba, 2024.
Katika maadhimisho hayo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kitatoa mafunzo
ya magari makubwa ya mizigo (HGV) mkoani Dodoma.
MUDA WA MAFUNZO
Tarehe ya Mafunzo:19/08/24 mpaka 31/08/24 (wiki mbili)
Siku za Mafunzo: Jumatatu mpaka Jumamosi
Muda wa Mafunzo: saa 2:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni
VIGEZO VYA KUJIUNGA
- Leseni daraja E iliyo hai na yenye uzoefu wa miaka miwili au zaidi
- Awe na Elimu ya Msingi au zaidi na aweze kusoma na kuandika
- Awe na umri usiopungua miaka 21
Kufaulu mtihani wa awali wa majaribio (pre-test) - Picha mbili (blue ground color)
MTIHANI WA AWALI (PRE-TEST)
Mtihani huu ni lazima na utafanyika kabla ya kujiunga na mafunzo
Siku ya mtihani ni Ijumaa 16/08/2024 na Jumamosi 17/08/2024
Muda wa mtihani ni saa 2:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni.
MTIHANI WA MWISHO: Utafanyika mwisho wa mafunzo kwa njia ya nadharia (theory) na vitendo
(practical).
GHARAMA ZA MAFUNZO: Ada ya Mtihani wa Awali (Pre-Test): TZS. 20,000
Ada ya mafunzo: TZS. 300,0000
MUDA NA NAMNA YA KUJISAJILI: Usajili upo wazi mpaka tarehe 19/08/2024.
Usajili unafanyika kwa njia zifuatazo:
Kupitia Wakala wa NIT Dodoma Driving School (+255 767 711 893) au
NIT Dar-es-Salaam (+255 757 077 439)
NAMNA YA KUFANYA MALIPO
Malipo yote yatafanyika kwa njia ya control number utakayopatiwa.
CHETI CHA UHITIMU
Cheti cha HGV kitatolewa kwa wale wote watakaokidhi vigezo ikiwemo kufaulu mtihani wa mwisho (Nadharia na Vitendo).
MAWASILIANO
Kwa maelezo ya zaidi kuhusiana na kozi hii wasiliana na Mratibu wa Mafuzo kupitia namba: (+255 752 521 641)