Pa Omar Jobe Apewa Thank You
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Pa Omar Jobe Apewa Thank You
Pa Omar Jobe Apewa Thank You,Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mshambuliaji, Pa Omar Jobe baada ya kipindi kifupi cha miezi sita.
Jobe raia wa Gambia mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Simba katika dirisha la usajili la mwezi Januari akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya Zhenis inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan.
Jobe ni mmoja ya washambuliaji bora na mwenye uwezo mkubwa lakini ameshindwa kuendana na kasi na malengo ya Simba SC.
Katika kipindi chote alichokuwa na Simba Jobe alikuwa mchezaji msikivu mwenye nidhamu ya hali ya juu na alikuwa anajituma mazoezini na uwanjani.
Kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/2025 Simba inafanya marekebisho makubwa ya kikosi kwani malengo yao ni kurejesha makali ambayo timu likuwa nayo miaka minne iliyopita.
Simba inamtakia kheri Jobe katika maisha mapya ya soka nje ya Simba.