PRINCE Dube Kutua Yanga ni suala la Muda
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
PRINCE Dube na Yanga ni suala ya Muda
PRINCE Dube na Yanga ni suala ya Muda, Taarifa za uhakika ambazo Nijuze Habari imezipata mshambuliaji, Prince Dube tayari amemalizana na Klabu ya Azam FC baada ya kulipa fedha alizokuwa anadaiwa na klabu hiyo na anachosubiri sasa ni ‘release letter’
Azam Fc wameahidi watampatia barua hiyo wiki ijayo ambapo baada ya kuipata, itamtambulisha kuwa ni mchezaji huru.
Baada ya hatua hiyo, Yanga itakuwa huru kumtambulisha kama mchezaji wake kwani Nijuze Habari inajua kuwa Dube tayari amesaini mkataba wa miaka miwili pale Jangwani.
Wakati akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili mkoani Morogoro kwenye tamasha la wape tabasamu, Dube alidokeza kuwa msimu ujao ataendelea kuonekana katika Ligi Kuu ya NBC (Mungu akipenda) lakini hakuwa tayari kuitaja timu atakayojiunga nayo.
Dube alijiunga na Azam FC Agosti 2020, akitokea Highlanders ya Zimbabwe kwa kusaini mkataba wa miaka miwili hadi 2022.
Mwaka 2021 akasaini nyongeza ya mkataba hadi 2024 na huo ndio mkataba ambao Dube alikuwa anadai kuutambua kabla mambo hayajabadilika.
Lakini Azam walikuwawa wanasisitiza kuwa, mwaka jana nyota huyo wa kimataifa wa Zimbabwe alisaini tena mkataba hadi 2026.