RAIS Mhe. Dkt. Samia Ateua na Kutengua July 21-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
RAIS Mhe. Dkt. Samia Ateua na Kutengua July 21-2024
RAIS Mhe. Dkt. Samia Ateua na Kutengua July 21-2024,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo:-
✅Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
✅Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
✅Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
✅Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Yusuf Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
✅Mhe. Cosato David Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
✅Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
✅Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
✅Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
✅Bi. Mary Gaspar Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu Madenge ambaye amestaafu;
✅Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
✅Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
✅Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
✅Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
✅Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
✅Dkt. Maulid Suleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
✅Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa; na
✅Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).