RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


RAIS Samia afanya Uteuzi na Uhamisho wa Viongozi

Filed in Habari by on 03/09/2024 0 Comments
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

RAIS Samia afanya Uteuzi na Uhamisho wa Viongozi

RAIS Samia afanya Uteuzi na Uhamisho wa Viongozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo:-

Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya
Luteni Kanali Fredrick Faustin Komba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji;

Bw. Mohamed Mussa Mtulyakwaku ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mtulyakwaku alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba; na

Bw. Olivanues Paul Thomas ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Thomas alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia.

Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya
Mhe. Halima Habib Okash amehamishwa kutoka Wilaya ya Bagamoyo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba;

Mhe. Gerald Romuald Mongella amehamishwa kutoka Wilaya ya Chemba kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua;

Mhe. Dkt. Rashid Mohamed Chuachua amehamishwa kutoka Wilaya ya Kaliua kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma;

Mhe. Salum Hamis Abdallah Kali amehamishwa kutoka Wilaya ya Kigoma kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido;

Mhe. Shaibu Issa Ndemanga amehamishwa kutoka Wilaya ya Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo;

Mhe. Victoria Charles Mwanziva amehamishwa kutoka Wilaya ya Ludewa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi;

Mhe. Abdallah Mussa Mwaipaya amehamishwa kutoka Wilaya ya Mwanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara;

Mhe. Mwanahamisi Athumani Mukunda amehamishwa kutoka Wilaya ya Mtwara kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga;

Mhe. Emmanuela Kaganda Mtatifikolo amehamishwa kutoka Wilaya ya Arumeru kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati;

Mhe. Lazaro Jacob Twange amehamishwa kutoka Wilaya ya Babati kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai;

Mhe. Amir Mohamed Mkalipa amehamishwa kutoka Wilaya ya Hai kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru;

Mhe. Dkt. Khalfan Boniface Haule amehamishwa kutoka Wilaya ya Musoma kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya;

Mhe. Juma Issa Chikoka amehamishwa kutoka Wilaya ya Rorya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma; na

Mhe. Zakaria Saili Mwansasu amehamishwa kutoka Wilaya ya Uyui kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe.

Uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya
Bw. Mohamed Juma Ngasinda ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba; na

Bw. Shabani Shabani Hamimu ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia.

Uhamisho wa Makatibu Tawala wa Wilaya
Bi. Warda Abdallah Obathany amehamishwa kutoka Wilaya ya Iramba kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni; na

Bi. Stella Edward Msofe amehamishwa kutoka Wilaya ya Kinondoni kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba.

Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
Bi. Hanan Mohamed Bafagh amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti; na

Bw. Hemedi Said Magaro amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Uteuzi wa Wakuu wa Taasisi na Mwenyekiti wa Bodi
Bw. Mick Lutechura Kiliba ameteuliwa kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kiliba alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;

Bw. Macrice Daniel Mbodo ameteuliwa kuwa Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania (TPC); na

Bw. Eliud Betri Sanga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *