RAIS Samia Afanya Uteuzi Tume Ya Mipango TAEC na NACTVET
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
RAIS Samia Afanya Uteuzi Tume Ya Mipango TAEC na NACTVET
RAIS Samia Afanya Uteuzi Tume Ya Mipango TAEC na NACTVET, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Mursali Ally Milanzi kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Mipango ya Kitaifa.
Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Milanzi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Kitaifa katika Tume ya Mipango.
Rais Dkt. Samia pia amemteua Dkt. Lorah Basolile Madete kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Ubunifu wa Biashara.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Madete alikuwa Meneja wa Idara ya Uchumi Benki Kuu ya Tanzania, Tawi la Mwanza.
Katika hatua nyingine Rais Samia amemteua Dkt. Linda Ezekiel kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Menejimenti ya Utendaji na Tathmini.
Dkt. Ezekiel alikuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, President’s Delivery Bureau (PDB).
Aidha Dkt. Samia amemteua Bw. Alban Mark Kihulla kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Kihulla alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Rais Samia amemteua Prof. Najat Kassim Mohamed kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC).
Kabla ya uteuzi huu Prof. Najat alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo (Mipango, Utawala na Fedha), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).
Vilevile Dkt. Samia amemteua Bi. Bernadetta Nagonyani Ndunguru kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).
Bi. Bernadetta ni Mkurugenzi wa Mafunzo Mstaafu, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: RAIS Samia Afanya Uteuzi Tume Ya Mipango TAEC na NACTVET