RASMI Clatous Chama ni Mwananchi
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
RASMI Clatous Chama ni Mwananchi
RASMI Clatous Chama ni Mwananchi, Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha saini ya aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Clatous Chota Chama raia wa Zambia mwenye umri wa miaka 33.
Chama ambaye kiwango chake kimekuwa kivutio machoni mwa
watazamaji amejiunga na Yanga kama Mchezaji huru akitokea kwa watani zao wa jadi Simba SC.
Kiungo huyo ambaye ana uzoefu na soka la Tanzania, alianza kuonyesha uwezo wake hapa nchini mwaka 2018 alipotua kwa mara ya kwanza.
Ujio wa Chama katika kikosi Yanga unaongeza wigo mpana katika eneo la
kiungo cha ushambuliaji akiwa
sambamba na Viungo wengine ambao Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki.
Haya ni maboresho ya kikosi Cha Young Africans katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa kuelekea msimu ujao wa 2024-2025 yakiwa malengo yao ni kutetea mataji yote waliyobeba msimu wa 2023-2024 ambayo ni Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Bank Federation huku pia wakihitaji kufanya vizuri zaidi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuishia robo fainali msimu uliopita.
Huu unakuwa usajili wa kwanza kukamilika Kwa Yanga huku pia Maboresho zaidi yakiendelea kuanzia Leo July 01-2024.