RASMI Moussa Camara Atambulishwa Simba SC
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
RASMI Moussa Camara Atambulishwa Simba SC
RASMI Moussa Camara Atambulishwa Simba SC, Mlinda mlango mahiri, Moussa Camara amejiunga na Simba SC Kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Horoya Athletic Club.
Camara raia wa Guinea mwenye umri wa miaka 25 anatua Simba kuongeza nguvu katika idara ya golikipa kwakuwa Simba inahitaji kufanya vizuri msimu ujao wa 2024/2025.
Baada ya kusaini mkataba, Camara amesema kuwa ana ushukuru Uongozi wa klabu hiyo kwa kumpa nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi hicho.
Camara amesema kuwa Simba ni timu kubwa na wachezaji wengi Afrika wana ndoto ya kuichezea kama ilivyo yeye kwake ni heshima kubwa.
“Namshukuru Mungu kuwa hapa, pia
nawashukuru Viongozi wa Simba kunipa nafasi na kuniamini kuwa naweza kuwa sehemu ya timu hii.”
“Nipo hapa kwa ajili ya kuhakikisha naisadia timu kufanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu,” amesema Camara.