RASMI Valentin Nouma ni Mnyama
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
RASMI Valentin Nouma ni Mnyama
RASMI Valentin Nouma ni Mnyama, Klabu ya Simba imekamilisha usajili mlinzi wa kushoto Valentin Nouma raia wa Burkina Faso kutoka klabu ya St. Eloi Lupopo ya DR Congo kwa mkataba wa miaka mitatu.
- USAJILI Omary Omary Atua SimbaValentin mwenye umri wa miaka 24 ana uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia kwa wakati mmoja.
Valentin ni mchezaji bora msimu wa 2022/2023 akishinda tuzo ya beki bora wa mwaka katika Ligi ya Burkinafaso alipokuwa akiichezea klabu ya AS Douanes.
Ubora mwingine aliokuwa nao Nouma ni kufunga kwa kutumia mipira ya adhabu pamoja na uwezo mkubwa wa kufunga mikwaju ya penati.
Kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/2025 Klabu hiyo inaboresha kikosi Chao katika kila idara ili kuwa na wachezaji wenye viwango vya hali ya juu.
Valentine anakuja kuongeza nguvu upande wa kushoto akisaidiana na Mohammed Hussein ambapo msimu uliopita alikua mchezaji pekee anayecheza nafasi hiyo.
Valentin Nouma anakuwa Mchezaji wa 10 kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa Wachezaji wengine ambao ni;
Omary Omary Kutoka Mashujaa FC, Debora Fernandes Mavambo Kutoka Mutondo Stars ya Zambia, Augustine Okejepha Kutoka Rivers United ya Nigeria, Valentino Mashaka Kutoka Geita Gold FC na Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini.
Wengine ni Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.