RATIBA ya Safari ya Simba chini Misri
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
RATIBA ya Safari ya Simba chini Misri
RATIBA ya Safari ya Simba chini Misri, Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kuwa kikosi Cha Simba kitaondoka leo saa 11 Jioni kuelekea Cairo nchini Misri tayari kwa kuanza kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2024/2025.
Ahmed amesema kuwa Leo July 08-2024 litaondoka kundi la kwanza la watu 30 na Julai 10 kundi la pili ambalo litakuwa na wachezaji wageni na watu wa benchi la ufundi ambao wamechelewa kupata visa.
Tazama kwenye video hapa chini Ahmed amekizungumzia ratiba Kamili ya safari hiyo pia kuhusu mlinda mlango Ayoub Lakred.
BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA RATIBA KAMILI YA SAFARI YA SIMBA
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohamed Dewji ‘Mo’ amekutana na benchi la ufundi na wachezaji na kufanya mazungumzo yenye lengo la kukumbushana malengo ya timu msimu huu wa 2014/2025.
Mo amesema ana kuwa matumaini makubwa na kikosi kilichosajiliwa pamoja na benchi la ufundi lililopo.
Aidha ameweka wazi kuwa malengo yake ni kuiona Simba inachukua Ubingwa wa Afrika na hilo linatakiwa kuwa kwenye vichwa vya wachezaji na siku zote wanatakiwa kujua hilo.
Pamoja na hilo Mo amewasisitiza wachezaji na benchi la ufundi lengo mama kwa sasa ni kuhakikisha Simba inarejesha mataji yote waliyopoteza katika miaka ya karibuni.
“Mimi pamoja na Bodi nzima ya Wakurugenzi tunawaamini nyinyi wote, na kila mmoja anatakiwa kufahamu Simba ni timu kubwa na ina mahitaji makubwa pia kwa hiyo anatakiwa ajitume ili kufanikisha malengo ya timu.”
“Siku ya kwanza wakati nimekuja kuwekeza katika klabu hii malengo yangu niliweka wazi kabisa kuwa ni kuiona Simba inachukua ubingwa wa Afrika hilo likitimia nafsi yangu itatulia na litawezekana kama wachezaji mtajitoa hadi mwisho kwenye kila mchezo,” amesema Mo.