RITA Mfumo wa Huduma za Vizazi na Vifo
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
RITA Mfumo wa Huduma za Vizazi na Vifo
RITA Mfumo wa Huduma za Vizazi na Vifo,Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) unapenda kuufahamisha Umma kwamba sasa unaweza kutuma maombi ya kupata huduma zifuatazo kwa njia ya Kidigitali (Online).
- 1. Cheti cha Kuzaliwa
- 2. Cheti cha kuzaliwa cha zamani kwenda kipya
- 3. Uhakiki wa cheti cha Kuzaliwa
- 4. Cheti cha Kifo
- 5. Cheti cha kifo cha zamani kwenda kipya
- 6. Uhakiki wa cheti cha Kifo
BOFYA HAPA KUPATA HUDUMA
Hii ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kujaza Fomu ya Maombi ya cheti cha kuzaliwa au kifo kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote.
Baada ya kujaza fomu ya maombi ya cheti cha kuzaliwa au kifo, atatakiwa kuichapisha (Print) na kuiwasilisha
pamoja na vielelezo vingine katika Ofisi ya Wilaya iliyo karibu naye kwaajili ya
kushughulikiwa maombi yake ya Cheti.
VIELELEZO VINAVYOHITAJIKA WAKATI WA UJAZAJI WA FOMU YA MAOMBI YA
CHETI CHA KUZALIWA.
- Tangazo la kizazi kwa vizazi vilivyosajiliwa ndani ya muda katika vituo vya tiba
- Kadi ya Kliniki
- Cheti cha ubatizo
- Pasi ya kusafiria
- Cheti cha kumaliza elimu ya msingi au secondari (leaving certificate)
- Kitambulisho cha Utaifa au Kadi ya kupigia kuraVitambulisho vya Utaifa au Kadi ya kupigia kura vya wazazi
- Picha ya Mwombaji ya hivi karibuni yenye kivuli cha rangi ya buluu isiyokoza (Light blue Background) Zingatia/Muhimu
Mwombaji lazima aambatishe vielelezo si chini ya viwili kati ya hivyo vilivyotajwa pamoja na vitambulisho vya wazazi.
VIELELEZO VINAVYOHITAJIKA WAKATI WA UJAZAJI WA FOMU YA MAOMBI YA
CHETI CHA KIFO
- Tangazo la kifo kwa kifo kilichoandikishwa ndani ya muda katika kituo cha tiba Kwa kifo kilichotokea nyumbani au kuchelewa kuandikishwa mwombaji aambatishe
BARUA YA UTAMBULISHO: Mwombaji wa cheti cha kifo kilichochelewa
kuandikishwa anatakiwa kuleta barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa
Mtendaji wa Kata/kijiji wa eneo tukio lilipotokea. Barua hiyo inatakiwa itaje
majina kamili ya marehemu, tarehe ya kifo, mahali alipofia na sababu za
kifo. Vilevile picha ndogo ya Mwombaji iweke kwenye barua hiyo na
igongwe muhuri.
MUHTASARI WA KIKAO CHA WANANDUGU: Ndugu wa marehemu
wanatakiwa wakae kikao na kuandaa muhtasari ambao una agenda za
kikao ambazo pamoja na mambo mengine ni kumteua msimamizi wa
mirathi ambaye ndiye atakayetambulika kisheria kufuatilia cheti cha kifo.
Kikao kihudhuriwe na ndugu wa marehemu. Pia watatakiwa kuorodhesha
majina yao na kuonyesha uhusiano wao na marehemu.
Ndugu haowatatakiwa waweke sahihi kuthibitisha ushiriki wao.
Muhtasari huuu thibitishwe na Afisa Mtendaji wa Kata/kijiji kwa kugonwa muhuri nak uweka sahihi yake.
ANGALIZO: Ifahamike kuwa muhtasari huo unatakiwa ushirikishe ndugu
wote wa karibu wa marehemu ili kuondoa migogoro inayoweza kutokea.
Pia endapo Msajili atakuwa na mashaka juu ya yaliyomo katika muhtasari
huo anaweza kuwaita baadhi ya waliohudhuria kwa mahojiano zaidi.
HATI YA KIAPO: Hati ya kiapo kutoka mahakamani au kwa mwanasheria
iliyoapiwa na mwombaji (Msimamizi wa Mirathi) na kueleza taarifa za marehemu kama majina kamili, tarehe ya kifo na mahali alipofia na sababu za kifo Uhakiki wa Vyeti vya Vizazi na Vifo
Hii ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kuwasilisha maombi ya kuhakiki cheti cha kuzaliwa na kifo kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote.
Muombaji atatakiwa kuscan cheti cha kuzaliwa au kifo anachohitaji kihakikiwe na kisha kukituma kwa njia ya kieletroniki ili kihakikiwe.
Majibu ya uhakiki yatatumwa katika akaunti uliyofungua sehemu iliyoandikwa ‘’View Status” Linki ya kuingia katika mfumo: https://erita.rita.go.tz/auth