RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

RUNGU la TFF Lawakuta Waamuzi, Gamondi apigwa Faini

Filed in Michezo by on 14/05/2024 0 Comments

RUNGU la TFF Lawakuta Waamuzi, Gamondi apigwa Faini

RUNGU la TFF Lawakuta Waamuzi, Gamondi apigwa Faini, Marefa Waliokataa Magoli waondolewa, Gamondi apigwa Faini, aliyekataa bao la Guede aondolewa Ligi Kuu.

RUNGU la TFF Lawakuta Waamuzi, Gamondi apigwa Faini

RUNGU la TFF Lawakuta Waamuzi, Gamondi apigwa Faini, Marefa Waliokataa Magoli waondolewa, Gamondi apigwa Faini, aliyekataa bao la Guede aondolewa Ligi Kuu.

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Mei 12, 2024 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Ligi Kuu ya NBC
Mechi Namba 193: KMC FC 0-0 Kagera FC

Klabu ya KMC imetozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuwakilishwa na maafisa wanne (4) badala ya watano (5) kwenye kikao cha kitaalam cha maandalizi ya mchezo (MCM) kuelekea mchezo tajwa hapo juu Mei 4, 2024.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:2(2.2) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi Namba 195: JKT Tanzania FC 2-0 Geita Gold FC

Klabu ya Geita Gold imetozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kukataa kutumia chumba maalum cha kuvalia kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Mei 4, 2024 kabla mchezo kuanza na wakati wa mapumziko.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:20 na 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Meneja wa timu ya Geita Gold, Abeid Choke amefungiwa michezo mitatu (3) kwa kosa kuongoza wachezaji wa timu hiyo katika tukio la kuvunja yai uwanjani, jambo lililohusianishwa na vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 45:2(2.4) ya Ligi Kuu.

Mechi Namba 200: Simba SC 2-0 Tabora United FC

Mwamuzi msaidizi namba moja wa mchezo tajwa hapo juu, Frank Chavala kutoka mkoani Morogoro, ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu kwenye uwanja wa Azm Complex Mei 6, 2024.

Mwamuzi huyo alikataa bao halali lililofungwa na mchezaji Najim Mussa wa klabu ya Tabora kwa tafsiri kuwa mpira haukuvuka mstari.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Mechi Namba 201: Young Africans SC 1-0 Kagera Sugar FC

Mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo tajwa hapo juu, Shaban Mussa kutoka Geita ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.

Mwamuzi huyo alikataa bao halali lililofungwa na mchezaji Joseph Guede wa klabu ya Yanga kwa tafsiri yake kuwa mchezaji huyo alikuwa ameotea.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Miguel Gamondi ametozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kufanya vurugu ikiwemo kuwashambulia kwa maneno makali waamuzi wa mchezo tajwa hapo juu.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 45:2(2.1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Mechi Namba 206: Mashujaa FC 3-0 KMC FC

Klabu ya KMC imetozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kukataa kutumia chumba maalum cha kuvalia kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma Mei 4, 2024 wakati wa mapumziko.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:20 na 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Ligi ya Championship ya NBC
Mechi Namba PO4: Transit Camp FC 1-1 Green Warriors FC

Klabu ya Transit Camp imetozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa kushindwa kuweka mabango 10 ya wadhamini kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Meja Jenerali Isamuhyo katika mchezo tajwa hapo juu kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni ya 16:1(1.5) ya Championship kuhusu Udhamini.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 47:28 ya Ligi ya Championship kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Wachezaji Abubakar Saad wa Transit Camp na Salum Hamis wa Green Warriors wametozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kila mmoja kwa kosa la kuchelewa kwa makusudi kurejea kiwanjani ili kuanza kipindi cha pili cha mchezo tajwa hapo juu.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 41:5 ya Ligi ya Championship kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

First League
Mechi Namba PO4: Kurugenzi FC vs Moro Kids FC

Klabu ya Moro Kids imepewa ushindi wa mabao matatu (3) na alama tatu (3) baada ya klabu ya Kurugenzi kushindwa kutokea uwanjani kuelekea mchezo tajwa hapo juu kwenye uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Klabu ya Kurugenzi imepoteza mchezo huo na imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 3,000,000 (milioni tatu) na kupokwa alama 15 katika msimamo wa Ligi ambayo klabu hiyo itashiriki.

Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 32:1(1.1, 1.2 & 1.3) ya First League kuhusu Kutofika uwanjani.

Tags: , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *