SAITI Mary Atinuke ni Mnyama
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
SAITI Mary Atinuke ni Mnyama
SAITI Mary Atinuke ni Mnyama, Klabu ya Simba Queens imekamilisha usajili wa Kiungo mkabaji Saiti Mary Atinuke Kutoka Yanga Princess kwa mkataba wa miaka miwili.
Atinuke ni raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 24 ambaye sifa yake kubwa ni kuipa timu uwiano wakati wa kuzuia na kushambulia.
Atinuke pia anaweza kucheza kiungo wa juu namba nane kwa ufanisi mkubwa.
Katika msimu uliopita amefanikiwa kufunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mengine mawili.
Atinuke anatua Simba Queens kuongeza nguvu kwenye kiungo wa ulinzi na kuisaidia timu kupandisha timu.