SIFA za Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
SIFA za Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura
SIFA za Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura, Kwa mujibu wa Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, ili mtu aweze kuandikishwa kuwa Mpiga Kura anatakiwa kuwa sifa zifuatazo:
- Awe Raia wa Tanzania;
- Awe ametimiza umri wa miaka 18 ; na
- Awe hajapoteza sifa kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 au Sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Bunge.
- Awe atatimiza umri wa miaka kumi na nane kabla au ifikapo siku ya uchaguzi;
- Awe ni mkazi wa kawaida katika jimbo au kata ambayo anaomba kuandikishwa;
- Awe na akili timamu;
- Awe hajatiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifo au hatumikii kifungo kwa kosa ambalo adhabu yake inazidi miezi sita;
- Awe hajawekwa kizuizini kwa amri ya Rais; na
- Awe hana utii wa nchi nyingine tofauti na Tanzania
Baada ya kutimiza Sifa hizi, mtu unatakiwa kufuata utaratibu ufuatao:
- Utaenda kituo cha kuandikisha Wapiga Kura kilichopo jirani na maeneo unayoishi.
- Utajitambulisha kwa Mwandishi Msaidizi na Mwandishi Msaidizi atakuuliza maswali na atakujazia fomu maalum
- Utaenda kwa BVR kit Operator kwaajili ya kuchukuliwa alama za kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupigwa picha
- Utapewa kadi ya Mpiga Kura na unatakiwa uihakiki majina yako, picha na taarifa nyingine, kama kipo sahihi na baada ya kujiridhisha utaondoka kituoni.