SIKU 5 Zaongezwa Maombi ya Ajira za Jeshi la Polisi May 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
SIKU 5 Zaongezwa Maombi ya Ajira za Jeshi la Polisi May 2024
SIKU 5 Zaongezwa Maombi ya Ajira za Jeshi la Polisi May 2024, Serikali yaongeza Siku 5 Kutuma Maombi Ajira za Jeshi la Polisi Tanzania May 2024, Kuomba Ajira za Jeshi la Polisi, Serikali yaongeza muda.
-
NAFASI za Kazi Kutoka Jeshi la Polisi Tanzania May 2024
-
JINSI ya Kutuma Maombi Ajira za Jeshi la Polisi Tanzania
-
MFANO Barua Ya Kuomba Kazi Jeshi La Polisi 2024
-
SERIKALI Kuajiri Walimu 12000 mwaka wa Fedha 2024
Serikali imeongeza siku tano (5) za kuomba Ajira kwenye Jeshi la Polisi Tanzania ambapo siku ya mwisho ilikuwa kesho May 16-2024.
Hayo yamesemwa Bungeni leo May 15-2024 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipokuwa akitoa Ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa Bungeni na Mbunge wa Makete, Festo Sanga aliyetumia kanuni namba 54 ya kutoa jambo la dharura Bungeni.
Kanuni hiyo inamruhusu Mbunge kuliomba Bunge kusimamisha shughuli zake na kujadili suala la dharura na kwa mujibu wa Sanga, ukosefu wa mtandao wa intaneti nchini umesababisha vijana wengi kushindwa kuingia kwenye Mtandao wa Polisi kuomba Ajira hizo.
Mwenyekiti wa Bunge, Deo Mwanyika ametoa mwongozo wa hoja hiyo kwa kuitaka Serikali kutoa maelezo ndipo, Waziri Msauni amelieleza Bunge kuwa baada ya kutokea tatizo la Inateti nchini wameamua kuongeza siku tano kuanzia kesho May 16-2024.
Masauni pia amesema iwapo changamoto ya intaneti itaendelea, Serikali itaangalia namna ya kufanya ili kuwasaidia waombaji kufikia malengo yao.
Pia, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye naye amelieleza Bunge kuwa mategenezo ya mtandao wa Intaneti hadi sasa yako asilimia 80 na kwamba hadi mchana itakuwa imetengemaa kwa asilimia 100.
Mnamo May 09-2024 Jeshi la Polisi lilitangaza ajira Nafasi mbalimbali za Ajira kwa Vijana wenye Elimu ya Shahada, Astashahada, Kidato cha Sita na cha Nne, huku moja ya sifa kwa muombaji lazima awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi makao makuu Dodoma May 09-2024, Miongoni mwa Nafasi hizo kwa upande wa shahada ni 74, Diploma 66 na upande wa ngazi ya Cheti (Astashahada ni 66).
Fani zinazotakiwa kwa kila ngazi ya Elimu ni pamoja na Uuguzi, Famasia, Uhandisi wa Vyombo vya Majini, Kompyuta, Muziki, Wapima Ardhi, Usimamizi wa Michezo na Utawala.
“Waombaji wanatakiwa waandike barua kwa mkono na wasisahau namba za simu na wanapaswa kutumia anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 Dodoma.
Aidha Waombaji wote wafanye maombi kupitia kwenye mfumo wa ajira wa Polisi (Tanzania Police Force -Recruitment Portal) unaopatikana kwenye tovuti ya jeshi hilo ya; www.polisi.go.tz na mwisho wa kupokea Maombi hayo ilikuwa May 16, 2024 Sasa itakuwa May 21-2024.
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
- Awe amehitimu kidato cha nne au sita kuanzia mwaka 2018 hadi 2023.
- Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
- Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne (Division I – IV). Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Point) 26 hadi 28.
- Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu (Division I – III)
- Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.
- Awe na urefu usiopunguwa futi tano na inchi nane (5’8”) kwa wanaume, na futi tano inchi nne (5’4”) kwa wanawake.
- Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).
- Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kingereza.
- Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
- Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
- Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya.
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
- Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
- Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
- Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili.
- Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
- Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
- Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8),
Stashahada (NTA level 6) na Astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa wawe na fani zilizoainishwa kwenye tangazo hili. - JINSI ya Kutuma Maombi Ajira za Jeshi la Polisi Tanzania
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
- Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (Handwriting) bila kusahau namba za simu na watumie anuani ya
Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA. - Waombaji wote wafanye maombi yao kupitia kwenye mfumo wa Ajira wa Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL)
unaopatikana kwenye tovuti ya Jeshi la Polisi ajira.tpf.go.tz
Mwisho wa Kupokea Maombi Sasa ni tarehe 21/05/2024 baada ya Kuongea Siku 5 Kutokana na Changamoto ya Internet.
DONWLOAD PDF DOCUMENT HAPA
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Kuomba Ajira za Jeshi la Polisi, Serikali yaongeza muda., Serikali yaongeza Siku 5 Kutuma Maombi Ajira za Jeshi la Polisi Tanzania May 2024, SIKU 5 Zaongezwa Maombi ya Ajira za Jeshi la Polisi May 2024
Kwa waliomaliza kidato cha nne 2023 bado namba za nida zinasumbua kutoka na dirisha ni la mda mfupi mnawasaidia je?
Nafasi ya uaskari
Naipenda sana kazi ya jeshi na nikipata nafasi nitaitumia vizuri sana..
Naipenda sana kazi ya polis tatizo mtandao jmn
Hereby Gati samson do apply job beyond jeshi
Mimi raia was mtanzania nimejitolea kuomba nafasi za ajira za police na vigezo vyote ninavyo naomba ombi langu likubaliwe
Naomba nafasi nikalitumikie taifa kwa uadilifu
Yes
Kisandupaskali:
Maombi ya kujiunga na jeshi la police Tanzania
Maombi ya kujiunga na jeshi la police Tanzania
Naipenda kazi ya polisi
Polisi military