SIMBA Kukutana na Uhamiaji au Bingwa wa FA Libya
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
SIMBA Kukutana na Uhamiaji au Bingwa wa FA Libya
SIMBA Kukutana na Uhamiaji au Bingwa wa FA Libya, Droo ya kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF Confederation Cup 2024/2025 hatua ya awali na hatua ya Kwanza imekamilika.
Simba itasubiri kucheza mechi ya raundi ya Kwanza kusaka nafasi ya Kutinga hatua ya Makundi mwezi September 2024.
Katika hatua hiyo ya kwanza ya CAF Confederation Cup 2025/2025, Simba SC imepangwa kukutana na mshindi wa mchezo wa hatua ya awali kati ya Uhamiaji FC ya Zanzibar au Bingwa wa FA chini Libya.
Ligi Kuu ya Libya bado haijamalizika Kwa jinsi hiyo timu zitakazoiwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya CAF bado hazijafahamika.
Mshindi wa jumla katika mchezo wa hatua ya kwanza kati ya Simba SC dhidi ya Uhamiaji au mshindi wa FA nchini Libya atajikatia tiketi ya kufuzu hatua ya Makundi CAF Confederation Cup 2024/2025.
Kwa Upande wa Wagosi wa Kaya Coastal Union wao wataanzia ugenini dhidi ya FC Bravo ya Angola na mshindi wa mchezo huo atakuna na FC Lupopo ya DR Congo.
Droo kamili ya hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup 2024/2025 tazama hapa Chini.