SIMBA Kutumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
SIMBA Kutumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha
SIMBA Kutumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Klabu ya Simba imethibitisha klabu hiyo inaweza kutumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha katika mechi zake za nyumbani Ligi Kuu ya NBC msimu ujao wa 2024/2025.
Bado uongozi wa Simba unaendelea kufanya tathmini na kama jambo hilo litakubaliwa na Bodi ya Wakurugenzi, ukarabati wa uwanja huo utaanza.
Hakuna uhakika kama Serikali itaruhusu uwanja wa Benjamin Mkapa kutumika katika mechi zote licha ya kuwa mchakato wa kufunga VAR unaendelea.
Hivo Simba inaweza kutumia dimba la Mkapa kwa baadhi ya mechi na mechi nyingine zote kupigwa Sheikh Amri Abeid.
Msimu uliomalizika Simba iilicheza mechi moja dhidi ya KMC katika uwanja huo na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Klabu hiyo inataka kutumia wingi wa mashabiki mkoani Arusha kuiongezea hamasa timu katika mechi za nyumbani.
Tathmini ya msimu uliopita imeonyesha mwamko wa mashabiki wa Dar ulikuwa mdogo ambapo mashabiki wachache walijitokeza kushuhudia mechi ambazo Simba ilicheza dimba la Azam Complex na Uhuru.