SIMBA Queens yapangwa Kundi B CECAFA 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
SIMBA Queens yapangwa Kundi B CECAFA 2024/2025
SIMBA Queens yapangwa Kundi B CECAFA 2024/2025, Timu ya Simba Queens imepangwa kundi B katika Michuano ya kufuzu Fainali za Afrika kwa Wanawake kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Simba Queens amepata tiketi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) msimu uliopita.
Timu tisa zimepangwa kwenye makundi mawili na Bingwa wa Michuano hiyo ataiwakilisha CECAFA kwenye Mashindano ya Afrika.
Kundi B ambalo Simba Queens ipo lina timu zifuatazo:
Simba Queens (Tanzania)
PVP Buyenzi (Burundi)
Kawempe Muslim (Uganda)
Fad Djibouti (Djibouti)
Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Agosti 17 na kumalizika Septemba 4 katika mji wa Addis Ababa nchini Ethiopia.
CAF Women’s Champions League Qualifies Draw – CECAFA 2024