Simba Yaachana na Freddy Michael
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na aliyekuwa mshambuliaji wake Freddy Michael Koublan ambaye hakukidhi mahitaji ya kocha Fadlu Davies.
Simba imefikia hatua hiyo baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji, Leonel Ateba kutoka USM Alger.
Baada ya kuachwa na Simba Freddy Michael ametua Katika Klabu ya USM Alger ambapo Leonel Ateba ametokea.
Usajili huo umebainishwa kuwa si wa kubadilishana wachezaji, kwani Simba imetumia zaidi ya Milioni 540 kukamilisha usajili wa Leonel Ateba.
Freddy Michael anakuwa mchezaji wa tatu kucheza Ligi Kuu ya nchini Algeria 2024/2025 akitokea Simba SC.
Wachezaji wengine ni Sadio Kanoute na Babacar Sarr waliojiunga na JS Kabylie inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba SC, Abdelhak Benchikha.
Soma na hii: KIKOSI cha Simba SC msimu huu wa 2024/2025