SIMBA Yaachana na Saido Ntibanzonkiza
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
SIMBA Yaachana na Saido Ntibanzonkiza
SIMBA Yaachana na Saido Ntibanzonkiza, Wachezaji Walioachwa na Simba SC 2024, Simba yamuacha Ntibanzonkiza, Saido Ntibanzonkiza aachana na Simba SC.
Kiungo Mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza hatokuwa sehemu ya kikosi Simba kwaajili ya msimu ujao wa 2024/2025 baada ya kumaliza mkataba wake.
Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu alichodumu Simba akitokea Geita Gold FC, Ntibazonkiza amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza akiwa mfungaji bora wa timu katika misimu yote miwili na klabu inathamini mchango wake.
Msimu wa 2022/23 Saido Ntibazonkiza alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufunga mabao 17 sawa na Fiston Mayele aliyekuwa Mchezaji wa Yanga, huku pia akiibuka kiungo Bora wa msimu huo.
Licha ya kucheza kwa muda mfupi
Ntibazonkiza ameacha alama ndani ya Klabu ya Simba kutokana utumishi uliotukuka ndani na nje ya uwanja.
Uongozi wa klabu umemtakia kheri Ntibazonkiza katika maisha yake mapya ya soka nje ya timu ya Simba.
Kuachana na Saido Ntibanzokiza ni hatua za klabu Simba kuendelea kufanya maboresho makubwa ya kikosi kwaajili ya msimu ujao wa 2024/2025.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Saido Ntibanzonkiza aachana na Simba SC., SIMBA Yaachana na Saido Ntibanzonkiza, Simba yamuacha Ntibanzonkiza, Wachezaji Walioachwa na Simba SC 2024