Simba yatoa taarifa jeraha la Joshua Mutale
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Klabu ya Simba imethibitisha kuwa winga wake, Joshua Mutale alipata tatizo la nyama za paja ‘hamstring injury’ katika mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Tabora United uliopigwa uwanja wa KMC Complex juzi na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Daktari wa Simba Edwin Kagabo amebainisha kuwa tayari mchezaji huyo amepatiwa matibabu ya awali huku akisubiri uchunguzi zaidi wa jeraha hilo ambao utakamilika baada ya saa 48.
Hata hivyo Dk Kagabo amesema haionekani kama jeraha hilo ni kubwa sana, pengine anaweza kukaa nje kwa siku chache.
Katika hatua nyingine, kikosi cha Simba kimerejea mazoezini leo Jumanne kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa pili wa Ligi kuu dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa Jumapili ya August 25 katika uwanja wa KMC Complex Jijini Dar Es Salaam.