SIMBA Yatoa Tamko Ishu ya Kibu Denis
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
SIMBA Yatoa Tamko Ishu ya Kibu Denis
SIMBA Yatoa Tamko Ishu ya Kibu Denis, Klabu ya Simba imetoa taarifa kwa Umma kuwa mchezaji wake, Kibu Denis Prosper hajaripoti kambini kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024/2025.
Katika taarifa yake Simba imesema kuwa ilimuongezea Kibu mkataba wa miaka miwili zaidi utakaoisha, Juni 2026 na kumlipa stahiki zake zote za kimkataba.
Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akitoa sababu kadha wa kadha inazomfanya kushindwa kuripoti kambini.
Kutokana na utovu huo wa kinidhamu klabu itamchukulia hatua stahiki za kinidhamu na umma utapewa taarifa.