SIMBA Yawasili Salama nchini
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
SIMBA Yawasili Salama nchini
SIMBA Yawasili Salama nchini, Nahodha wa timu hiyo, Mohamed Hussein amesema kuwa kambi ya Misri ilikuwa Bora na wamepata maandalizi mazuri kuelekea msimu mpya wa 2024/2025.
Hussein ameyasema hayo muda mfupi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kutokea nchini Misri ambapo timu hiyo ilikuwa imeweka kambi ya wiki tatu.
Mlinzi huyo wa kushoto ameongeza kuwa kambi ilikuwa tulivu na wamepata kila kitu walichohitaji kilichobaki ni kwenda kukionyesha kwa vitendo uwanjani.
“Kambi ilikuwa nzuri, tunamshukuru Mungu tumerejea nchini salama tukiwa na nguvu ya kuwaonyesha Wanasimba kile tulichokifuata Misri,” amesema Zimbwe Jr.
Akizungumzia kuhusu wachezaji wapya
waliosajiliwa msimu huu, Hussein amesema kuwa “ni wachezaji wazuri wameonyesha wana kitu kikubwa watakiongeza kwenye timu ila sisi wakongwe huwa tunawaelekeza mipango na kinachohitajika kwa sasa.”