STEVEN Mukwala ni Mnyama
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
STEVEN Mukwala ni Mnyama
STEVEN Mukwala ni Mnyama, Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Steven Mukwala raia wa Uganda kutoka Asante Kotoko ya Ghana kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mukwala mwenye umri wa miaka 24 ni Mshambuliaji kinara mwenye uwezo wa kufunga hivo Simba inategemea atakuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi.
Mukwala amefunga mabao 14 na kuisaidia kupatikana kwa mengine mawili katika michezo 28 katika ligi kuu ya Ghana msimu wa 2023/2024.
Aidha Mukwala ana urefu wa futi 5.9 na ana uwezo wa kufunga magoli ya aina yeyote lakini pia ni mzuri kwenye mipira ya juu na mipira ya krosi na pia hivyo anatarajiwa atakuwa msaada mkubwa kwa Simba SC.
Moja ya eneo ambalo lilikuwa na mapungufu msimu uliopita Kwa Simba SC ni katika safu ya Ushambuliaji hivo ujio wa Mukwala utaongeza uimara wa timu akisaidiana na Fredy Michael Kouablan.
Mukwala amewahi kuzitumikia timu za Vipers FC, Maroons FC zote za Uganda kabla ya kutimkia Asante Kotoko ya Ghana.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: STEVEN Mukwala ni Mnyama