TAARIFA Kutoka HESLB Kuhusu Malipo ya Fedha za Kujikimu
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
TAARIFA Kutoka HESLB Kuhusu Malipo ya Fedha za Kujikimu
TAARIFA Kutoka HESLB Kuhusu Malipo ya Fedha za Kujikimu, Taarifa Kutoka Bodi ya Mikopo HESLB Kuhusu Malipo ya Fedha za Kujikimu Kwa Robo ya Nne, UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA FEDHA ZA KUJIKIMU KWA ROBO YA NNE.
HESLB imetoa taarifa kwa Wanafunzi Wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya juu na Umma kuwa inakamilisha Malipo ya Fedha za Kujikimu (Chakula na Malazi) kwa Robo ya nne (Quarter IV) hivo Wanafunzi watarajie kupokea Fedha hizo kuanzia Jumatatu ya May 20-2024.
Bodi hiyo imetoa ufafanuzi huo kufuatia maoni na Maswali yanayoulizwa na Wanafunzi wanufaika kupitia barua pepe, mitandao ya kijamii kuhusu hatua ya malipo iliyofikiwa hususan kwa Vyuo ambavyo tarehe za malipo (due dates) ya robo ya nne zimefika.
Bodi hiyo inawasihi Wanafunzi kuendelea kuwa watulivu na kuwasiliana na Maafisa Mikopo waliopo katika Vyuo vyote nchini pale watakapokuwa na maoni au kuhitaji Ufafanuzi zaidi.
Aidha, Katika mwaka wa masomo 2023/2024, Serikali imetenga TZS 786 bilioni kwaajili ya mikopo na ruzuku kwa Wanafunzi zaidi ya 220,000 wanaosoma Shahada na Stashahada Mbalimbali katika taasisi za Elimu nchini.
UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA FEDHA ZA KUJIKIMU KWA ROBO YA NNE
The Higher Education Students’ Loans Board (HESLB) is a body corporate established under Act No.9 of 2004 (as amended in 2007, 2014 and 2016) with the objective of assisting needy and eligible Tanzania students to access loans and grants for higher education. The main mandates of HESLB include:
To assist, on a loan basis, needy students who secure admission in accredited higher learning institutions, but who have no economic power to pay for the costs of their education
To collect due loans from loan beneficiaries and use it as revolving fund to sustain operations of the Board
To create synergies through establishing strategic partnerships in student financing ecosystem.