TAARIFA Rasmi ya Kambi ya Yanga 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
TAARIFA Rasmi ya Kambi ya Yanga 2024/2025
TAARIFA Rasmi ya Kambi ya Yanga 2024/2025,Klabu ya Young Africans Wachezaji kuanza kuripoti kambini kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2024-2025 Jumatatu ya Julai 08-2024.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe, amesema kuwa siku hiyo wachezaji wote wakiwemo wapya na wale wa zamani watatakiwa kufika Avic Town kwaajili ya kukutana.
Baada ya hapo, benchi la ufundi la Young Africans SC chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, litaanza mikakati ya kuiandaa timu.
Klabu hiyo imejiwekea malengo makubwa zaidi msimu ujao wa 2024/2025 ambayo ni kutetea mataji mawili ya Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Federation iliyobeba 2023-2024, pamoja na kubeba taji la Ngao ya Jamii.
Mbali na hayo, pia Klabu hiyo imejiwekea malengo ya kufika mbali zaidi katika michango ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya msimu uliopita kuishia Robo Fainali.